18 February 2013

Serikali kuboresha TBS



Na Grace Ndossa

SERIKALI imesema kuwa inaangalia uwezo wa kuboresha Shirika la viwango Tanzania ili waweze kufanya kazi kwa ubora na umahiri unaotakiwa.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)Bw.Leandri Kinabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  wakati Maseneta na Wawakili wa bunge la Nigeria walipotembelea TBS.

Alisema kuwa lengo la masenata hao pamoja na wawakili ni kujifunza sheria mpya ya TBS inapofanyakazi na namana wanapodhibiti bidhaa ambazo hazina viwango.

"Masenata na wawakilishi wa bunge la Nigeria walikuja kwa lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kujifunza njia mbali mbali wanazotumia katika kudhibiti viwango vya ubora wa bidhaa hapa nchini,"alisema Bw. Kinabo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango wa Nigeria Dkt.Joseph Odumodu alisema kuwa lengo la ziara ya siku tatu ya masenata na wabunge wa nigeria ni kujifu7nza pamoja na kuimarisha ushirikina baina  ya nchoi moja na nyingine.

Pia alisema Tanzania ni nchi mojawapo inayofanya vizuri katika kudhibiti viwango vya ubora  na nchi nyingine ni Ethiopia pamoja na  Kenya ambazo watatembelea na kupata mbinu mbali mbali za kudhibiti bidhaa feki zinazoingizwa nchini.

Hata hivyo alisema kuwa wanaangali ni kwa jinsi gani watashirikiana katika kufanya biasahara na kudhibiti uborawa viwango vya bidhaa zinazozalishwa ili ziwezekuwa na  viwango sawa.

No comments:

Post a Comment