18 February 2013

MAUAJI Z'BAR.PDRI MWINGINE APIGWA RISASI TATU KICHWANI.TIMU YA MAKACHERO YATUMWA,JK AOMBELEZA.WATATU MBARONI,WAUMINI WAANGUA KILIO

Mwajuma Juma na Goodluck Hongo

PADRI wa Kanisa Katoliki la Minara Miwili, lililopo Mji Mkongwe, Zanzibar, Evaristus Mushi, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi tatu kichwani na watu wasiofahamika jana asubuhi.


Tukio la mauaji hayo limeibua simanzi kubwa kwa waumini wa kanisa hilo ambao jana walikusanyika kanisani hapo baadhi yao wakilia, kulaani mauaji ya kinyama aliyofanyiwa kiongozi huyo.

Baadhi ya waumini hao, walihoji utekelezwaji wa tamko la Serikali baada ya Padri wa kanisa hilo, Parokia ya Mpendaye mjini Zanzibar, Ambrose Mkenda, kujeruhiwa kwa risasi Desemba 24,2012 na watu wasiofahamika akiwa nje ya nyumba yake.

Baada ya tukio hilo, Desemba 28,2012 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ilitoa tamko la kufanya uchunguzi wa kina
dhidi ya mfululizo wa matukio ya kushambuliwa viongozi wa
dini ili kubaini kama ni hujuma zinazofanywa na baadhi
ya watu wanaotaka kuifanya Zanzibar isitawalike.

Tamko hilo lilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohammed Aboud Mohamed, baada ya kumjulia hali Padri Mkenda, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).

Taarifa zilizolifikia gazeti hili, zinasema Padri Mushi alivamiwa
na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki aina ya Vespa, baada
ya kushuka katika gari lake ili kwenye Kanisa la Betras.

Baada ya tukio hilo, Padri Mushi alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja lakini baadaye alifariki dunia.

Rais Kikwete

Kutokana na tukio hilo, Rais Jakaya Kikwete, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina na haraka ili kuwabaini wahusika waliofanya tukio hilo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilisema Rais Kikwete amelitaja
jeshi hilo kushirikiana na vyombo vingine vya usalama nchini
na mashirika ya upepelezi kutoka nchi rafiki ili kufanya
uchunguzi wa mauaji hayo.

“Nataka umma ufahamu ukweli ili kama kuna jambo lolote
zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina, nimepokea
taarifa za mauaji haya kwa mshtuko na masikitiko makubwa.

“Naomba nitumie fursa hii kutuma salamu za rambirambi kwa
Baba Askofu, Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba mkubwa
ambao umewakuta,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza;

“Napenda kuwahakikishia kuwa, tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa wetu Padri Mushi...msiba huu ni wetu sote,” alisema Rais Kikwete.

IGP Mwema azungumza

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, Alisema Makao Makuu ya jeshi hilo Dar es Salaam, limepeleka timu ya wataalamu waliobobea katika masuala ya upelelezi na opereshini mjini Zanzibar.

Alisema wataalamu hao watashirikiana na wenzao waliopo Zanzibar ili kufanya uchunguzi wa kina juu ya mauaji ya Padri Mushi pamoja na kutumia fursa hiyo kulaani kitendo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, IGP Mwema alisema hadi jana mchana, jeshi hilo lilikuwa linawashikilia watu watatu ambapo timu ya watalamu hao, inaongozwa na Makamishna watatu.

“Naibu Kamishna wa Polisi Peter Kivuyo, atahusika kukusanya taarifa za matukio, Naibu Kamishna Samson Kasela ambaye atahusika na masuala ya upelelezi wakati Mkuu wa Operesheni
wa jeshi hilo, Simon Sirro atahusika na operesheni.

“Nawaomba wananchi wote mtusaidie kutoa taarifa juu ya watu wanaofadhili makundi yanayovuruga amani ya nchi, kuchochea
na kushawishi...huu ndio mkakati mpya wa jeshi letu ambao umeazimiwa mkoani Dodoma,” alisema IGP Mwema.

Aliongeza kuwa, hivi sasa jeshi hilo limeimarisha doria katika maeneo yote nchini, kufuatilia mienendo ya watu wanaochochea, kufadhiri, kuhamasisha na kushiriki vitendo vya uhalifu, vurugu na fujo hivyo aliwataka wananchi kuwa watulivu.

IGP Mwema aliwataka wananchi wote wenye taarifa ambazo zitasaidia kukamatwa wahalifu hao, wapige namba 0754 785557,
0782 417247 au kuwapigia makamanda wa vikosi ili kuhakikisha
amani, usalama na utulivu vinadumishwa nchini.

Waziri Mkuu Pinda

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, jana alikutana na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo mkoani
Geita na kuwataka watumie mkutano huo kwa manufaa ya Taifa 
ili kuleta amani na utulivu nchini.

Alisema tukio la kuuawa Padri Mushi huko Zanzibar, limemsikitisha sana na kuongeza kuwa, huenda likawa na uhusiano na vurugu zilizotokea mkoano Geita, kati ya Waislamu na Wakristo.

Mashuhuda wa tukio

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo, walisema Padri Mushi huwa na kawaida ya kwenda kusalisha katika Kanisa la Mtoni na alipofika kanisani hapo wakati akipaki gari lake, ghafla walitokea watu wawili, kumpiga risasi na kukimbia kusikojulikana.

“Hili kanisa lipo njiani kabisa, wakati tukipita tulisikia milio ya risasi...tulisogelea eneo husika la tukio na kukuta Padri Mushi akitokwa na damu nyingi kichwani,” walisema mashuhuda hao.

Waumini wake

Wakizungumza kwa masikitiko makubwa, waumini wa kanisa
hilo walisikitishwa na mauaji hayo na kuiiomba Serikali ifanye uchunguzi wa kina ili wahusika waweze kukamatwa.

“Tumetoka nyumbani tukiwa na matumaini makubwa ya kufanya ibada na Padri Mushi lakini tulipofika kanisani tukapata taarifa za kusikitisha...mbona Zanzibar haina amani tena maana tumeingiwa hofu ya kuendelea kuishi hapa visiwani,” walisema.

Mwili wa Padri Mushi umehifadhiwa katika mochali ya Hospitali Kuu Mnazi Mmoja. Kiongozi mwingine wa dini aliyefanyiwa unyama hivi karibuni ni Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Shekhe Fadhil Soraga, aliyemwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

Matukio ya viongozi wa dini kushambuliwa, yametanguliwa na uchomwa moto baa 12 na makanisa 25, katika maeneo tofauti visiwani Zanzibar.

9 comments:

  1. Ndugu muheshimiwa, aslam aley kum.
    1.Uchunguzi wa kumwagiwa tindikali kwa shehe wetu umeishia wapi?
    2. Na yule daktari aliyepigwa umepotelea wapi?
    3. Yule padri mkenda, vipi wamekamatwa?
    4. Makachero si walienda pia?
    tell us mheshimiwa, dekozi kuuana hakuna kikundi kinachoshindwa. Tukumbuke kuwa watanzania tunaishi nyumba za kupanga tukianza chuki hizi ujue nchi haitatawallika.
    Cha maana maelezo yatolewe, nani kakamatwa, walitumwa na nani?
    hatima yao ni nini na wapi?
    EE MWENYEZI MUNGU, TUEPUSHE NA BALAA HILI LA DHULMA NA MAUAJI YA NDUGU ZETU, BILA WEWE SISI WAJA WAKO HATUWEZI KITU, WACHUKUE WALE WOTE WANAOTAKA KUTULETEA DHULMA NA MAUAJI NA VITA, ILI WAJE KIAMANI ILI WALIOBAKI WAISHI KWA AMANI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kazi kwelikweli ifike mahari tumwogope mungu jamani hebu fikilieni mataifa jilani yanavyopata shida kutokana na vita asa nyie watu mnataka mwingize nchi hetu huko wakati tumebalikiwa amani ogopa sana vita ya kidini kwani ni ya mtu kwa mtu mungu ibariki tanzania mungu ibaliki zanzibar

      Delete
  2. Hawa watanzania wenzetu wa visiwani kwa muda mrefu wamekuwa wanaanza chokochoko sana ili kuvuruga amani nchi kwetu hivi hawa wanachokitafuta ni nini?? ndio maana walikuwa wanachinjwa kipindi cha mzee karume..tuombe mungu atunusuru na balaa la vurugu wanazozitafuta kwa uvumba na ubani hawa jamaa zetu wanaojiita wakereketwa wa uzanzibar.

    ReplyDelete
  3. Wanatuvurugia pasaka kama walivyosema. Kisasi ni cha Mungu kulipa lakini wakristo angalieni. Mnajega mashule, vyou vikuu, haopitali nk. Ndugu zetu hawa bado wanatuua! Alafu miaka kumi ijayo wanasema wakristo wameshika positions za juu. Kumbe kazi yao kuu ni kubomoa pale wenzao wanapojenga!! Tunahitaji kuwa wa wazi na yale tunayofanya na kusema kwa sauti ya juu maana ya wokovu wetu. Wasaidieni waislamu kwa kuwaambia ukweli, kuwaconfront na facts and kuwatia moyo wabadili fikra zao an kuthamini elimu, kazi na biddi kutenda mema.

    ReplyDelete
  4. Mnangojea serikali hii au ile ifanye nini? Kaeni mtathmini na kufanya initiative ninyi wenyewe. WaTZ tuna ugonjwa wa kungojea serikali ifanye, polisi wafanye nk. Angalia hata CCM wamekumbushwa juzi juzi tu kwamba si kungojea polisi bali jibuni mapigo kwa maelezo mazuri, nguvu za hoja na pia kuonyesha kwamba sis ni watu wazuri tusiopenda ujinga wa kuuana!

    ReplyDelete
  5. Raia wa zanzibar hawamiliki wala hawajawahi kumiliki silaha, waliyoyafanya haya na wanaoendelea kuyafanya ni watu kutoka bara kwa kuwa wao ndio wanaomiliki silaha kama alivyosema Kikwete kuwa Silhaha zinazotumika zanzibar zinatoka bara
    Inawezekana wauwaji ni wakristo wenyewe kwani kuna malalamiko kuwa, Wakristo wazanzib wanaletewa viongozi kutoka bara kwani wao hawawezi kuongoza?
    Waacheni Wazanzibari msiwatie midomoni na kuwatoa kwenye malengo, kwa sasa Malengo yao ni Kuikomboa zanzibar kutoka kwenye makucha ya Muungano.
    ZANZIBAR KWANZA

    ReplyDelete
    Replies
    1. 1.Maoni ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba huenda majahili yaliyomuua Padri Mushi yanatia kinyaa. Eti huenda yanahusiana na ubishi wa uchinjaji wa wanyama huko Geita! Kama hivyo ndivyo, atasema nini kuhusu majaribio yaliyotangulia ya kutaka kuondoa uhai wa Padri Nkenda mwaka jana? Awe huru.Kama hana cha kusema anyamaze. 2.Je,jeuri ya wauaji wa wakristo Zanzibar inatokana na mfumo wa idara za ulinzi na usalama za S/Muungano na za Serikali ya Mapinduzi? Ulinzi na usalama Zanzibar ni tata.Kwani licha ya polisi wa s/muungano , vipo vikosi kama jeshi la kujenga uchumi na grini belts. Hivi si vya serikali ya muungano. Ni vya serikali ya zanzibar! Ni vya nini? Vinaamrishwa na nani? Katika hali hiyo,amri za Mwema na Rais Kikwete kwa polisi wa s/muungano waliopo visiwani zitasaidiaje kudhibiti wanauamsho na majahili wengine wa visiwa hivyo? Vyombo vya habari vimesema kwamba baadhi ya viongozi visiwani wanachochea udini,eti! Tutafakari!

      Delete
  6. NI SIRI YA WAZI KUWA SERIKALI YA KIKWETE NDIYO INAENDEKEZA UDINI NA TENA KWA KUWAPENDELEA WAISLAMU NA MAANDAMANO YAO YASIYOISHA.
    VIONGOZI WA SERIKALI KUTOA POLE NI UNAFIKI NA UZANDIKI KWANI WAO NDIYO TATIZO KWA KUULEA UDINI.
    AIYUMKINI KUSEMA KUWA BAADHI YAO NDIYO WANAOFADHILI VIKUNDI HIVI VYA KUDINI VYENYE KULETA CHUKI NA CHOKO CHOKO.

    ReplyDelete
  7. tanzania hatuna viongozi bado tunahihitaji kutawliwa serikari iliyopo ni ya watu wachache wala si kwa ajili ya wananchi na ndio maana wannchi wanauliwa kila siku kuuwawa kwa mashehe au mapdri hay ni matokeo ya uongozi mbovu hakuna kiongozi shupavu wa kukemea haya yote. je kipindi cha mwalimu nyerere yangetokea haya ?

    ReplyDelete