05 February 2013

Mahakama ya watoto kuanzishwa Zanzibar



Na Mwajuma Juma, Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, inatarajia kufungua mahakama ya watoto ambayo itakuwa ikisikiliza kesi zao.

Jaji Mkuu wa Zanzibar, Bw. Omar Othman Makungu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu Siku ya Sheria ambayo itafanyika Februari 7
mwaka huu.

Alisema mahakama hiyo itakuwa ikisikiliza kesi za watoto walio chini ya umri wa miaka 18 na itazinduliwa kesho katika mahakama
ya Mkoa Vuga.

“Mahakama hii itakuwa na mahakimu maalumu pamoja na wanasheria ambao ambao watakuwa wakiendesha kesi zote zinazowahusu watoto,” alisema.

Aliongeza kuwa, kwa kuanzia watakuwa na mahakama moja katika Ofisi za Mahakama Mkoa na baadaye watafungua nyingine Kisiwani Pemba pamoja na maeneo yote ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment