18 February 2013
MAANDAMANO YA WAISLAMU Wafuasi 91 wa Ponda mbaroni *Walikuwa wamebeba fimbo, visu na mawe *Polisi wazima maandamano kwa mabomu
Rashid Mkwinda na David John
LICHA ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kutoa tamko la kuzuia maandamano ya wafuasi wa Katibu wa Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda pamoja
na mwenzake Shekhe Swalekh Mkadam, agizo hilo halikuweza
kuzuia dhamira ya wafuasi hao kuandamana.
Wafuasi hao, jana walijaribu kuandamana ili kufika katika Ofisi
ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), wakipinga viongozi
hao kuandelea kunyimwa dhamana mahakamani.
Kesi inayowahusisha viongozi hao na wafuasi wengine, ipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya kula njama ya kutenda kosa ambapo Oktoba 12,2012, wanadaiwa kuingia kwa nguvu katika eneo la Chang'ombe Markaz kwa jinai.
Eneo hilo linamilikiwa na Kampuni ya Agritanza ambapo kosa jingine ni kujimilikisha kiwanja hicho kwa njia iliyosababisha uvunjifu wa amani, wizi wa vifaa mbaolimbali vya ujenzi kama
nondo na kokote vyenye thamani ya sh. 59,650,000.
Gazeti hili liliwashuhudia wafuasi wa viongozi hao wakiandamana katika mitaa ya katikati ya jiji ambayo ni Kariakoo na Msimbazi wakiwa wameshika mawe na marungu mkononi.
Kundi hilo la vijana wakiwemo wanawake, walianza maandamano hayo katika maeneo ya Ilala Boma, kupitia Mchikichini hadi Kariakoo lakini walisambaratishwa na Jeshi la Polisi, kwenye
eneo la Kituo cha Mafuta Big Born.
Vijana hao walikuwa wakitamka maneno yanayosema “Takbiir Allah Akbar”, wakiwa na mabango yenye maneno yanayoshinikiza kuachiwa kwa Shekhe Ponda na mwenzake.
Jeshi la Polisi lilipiga mabomu ya mchozi ili kuwatawanya ambapo hali hiyo ilisabbisha taharuki kubwa kwa wafanyabiashara waliopo mitaa ya Kariakoo na Msimbazi.
Baadhi ya wafanyabiashara walilazimika kufunga maduka yao
na kukaa nje wakiwa wameshika chupa za maji ili waweze kuyatumia kwa kunawa uso ili kuondoa muwasho machoni
kutokana na mabomu yanayoweza kupigwa na polisi.
Awali katika Msikiti wa Idrisa uliiopoo Kariakoo, waumini wa dini hiyo walifanya ibada kwa tahadhari ambapo kuanzia saa sita mchana askari kanzu walikuwa maeneo jirani na Msikiti huo.
Mmoja wa viongozi wa msikiti huo alisimama na kusoma taarifa iliyosababisha waumini waamue kuandamana ili kwenda kwenye Ofisi ya DPP kushinikiza Shekhe Ponda na mwenzake waachiwe.
Kiongozi huyo alitumia kipaza sauti kusema kuwa, kama msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu', anayetuhumiwa kwa kosa la mauaji ameachiwa kwa dhamana iweje viongozi hao waendeleea kunyimwa dhamana wakati hawajaua.
Kamanda Msangi
Akizungumza na Majira, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ahmed Msangi, alisema jeshi hilo linawashikilia wafuasi 91 wa viongozi hao ambao walithubutu
kuandamana mbali ya maandamano hayo kuzuiwa.
Alisema wafuasi hao walijaribu kuandamana katika maeneo ya Buguruni, Kariakoo, Ilala na Barabara ya Kawawa wengine
wakiwa na visu, mabegi yaliyojaa mawe, fimbo na vipaza sauti.
“Tulifanikiwa kuwadhibiti kwa kuwatawanya na kuwakamata baadhi yao na miongoni mwao watafikishwa mahakamani, kati
ya waliokamatwa wanaume 88, wanawake wawili.
“Tunaendelea kuwachuja na vinara wa maandamano watafikishwa katika vyombo vya sheria, kimsingi walioandamana ni vikundi vya wahuni ambao wanajifanya Waislamu ili kuvuruga amani,” alisema.
Kamanda Msangi aliongeza kuwa, wahenga wanasema utii wa
sheria bila uhuru ni utumwa ambapo uhuru unapaswa kuwa na
mipaka hivyo aliwataka wananchi kulinda uhuru walionao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment