18 February 2013
Kwa nini habari za biashara hazipewe kipaumbele?
Na Yasinta Timoth
ASILIMIA kubwa ya magazeti ya Tanzania bado hayatoi kipaumbele kwa kuandika habari za mazingira bora ya biashara nchini hali inayochangiwa na utengaji wa habari za biashara, utaalamu wa masuala ya uandishi wa habari na ukosefu wa mafunzo.
Hayo yalibainishwa katika utafiti wa kutathimini ubora wa habari za uandishi wa habari za biashara kwa magazeti ya Tanzania ulifanyika 2012 na Taasisi ya kuboresha mazingira ya biashara nchini BEST- AC.Hali inaonesha kuwa kuna ubaguzi wa habari za biashara.
Ripoti ya inaonesha kuwa uhiano mdogo wa habari za biashara pia hazipewe kipaumbele kama habari nyingine, hali itayochangia kushindwa kuhabarisha taifa katika masuala ya ukuwaji wa uchumi na upatikaji wa nafasi za kazi.
Utaratibu wa vyombo vya habari wa kuzitenga habari za biashara, inachangia kwa asilimia kubwa ya waandishi wa habari, kuchagua matukio ya kuripoti na jinsi ya kuzipata taarifa hizo.
Hali ya kuripoti na kuegemea upande mmoja inaweza kujidhihirisha wakati wa kuisoma habari na kuichambua
Utafiti wa mwaka ulifanywa na Serengeti advisers limited baada ya kukabidhiwa na BESTT AC unaonesha kuwa habari ambazo zina ubora zimepungua ukilinganisha 2011.
Kwa mujibu wa utafiti huo unaonesha uandikaji wa habari za biashara umeboreshwa lakini bado hazifanyiwi uchunguzi wa kina ,hazipewe kipaumbele, hata aina ya vyanzo vyake vya habari ni vichache.
Pia utafiti huo uligundua kuwa habari za biashara zinazotolewa na magazeti ya Kiswahili zina bora mdogo ukilinganisha na zile zinatolewa na magazeti ya Kiingereza nchini.
Kwa mjibu wa Aidan Eyakuze ambaye ni Mkurugenzi wa wa Serengeti Adviser Limited Aidan Eyakuze, alisema asilimia 70 habari za biashara za Kiswahili zilipata alama mbaya wakati asilimia 30 ya habari za biashara za Kiingereza zilipata alama mbaya.
Anasema asilimia 30 ya habari za biashara za Kiswahili zilipata alama nzuri, na asilimia 71 ya habari za biashara za Kiingereza zilipata alama nzuri.
Anasema "Utafiti huo ulionesha kuwa bado uandishi wa habari za biashara zinaandikwa kutokana na maana na si umuhimu wake,"anasema
Mwaka 2008 BEST-AC ilikabidhi Serengeti Advisers Limited kufanya utafiti kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuchambuzi kama sekta ya habari Tanzania ni kikwazo cha kuboresha mazingira ya biashara Tanzania?
Anasema utafiti huo ulibaini kuwa katika miaka minne uandishi wa habari za mazingira bora ya biashara huripotiwa na magazeti sita yanayotoka kila siku.
Anasena mwaka 2012, sampo ya magazeti sita yalifanyiwa utafiti na kugundulika kuwa magazeti ya Kiswahili kwa ujumla hutoa habari za uchumi mkubwa,habari za biashara za kimataifa na habari chache ambazo zinawahusisha wajasiriamali wadogo.
Anasema vigezo vilivyotumika ni ukubwa wa habari , mfumo wa uandishi habari, uzito wake, ukurasa gani imewekwa na vyanzo vya habari vilivyotumia.
Utafiti huo uliwashirikisha
waandishi wa habari,mameneja wa vyombo vya habari wamiliki wa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa Eyakuze mwaka huu upungufu wa aina tatu umeshajitokeaza, vyombo vya habari ambavyo haviwezi kuwezesha waandishi wake wafanye habari za utafiti ndio wanatoa habari za biashara.
Anasema Mfuko wa Sekta Binafsi hauna utaalamu wa kutoa taarifa na kuishauri serikali kupitia wizara husika na wakala wa masuala ya biashara hawana uelewa unaotakiwa.
Eyakuze anasema kuna vitengo vimeanzishwa vya mahusiano lakini serikali inaficha taarifa muhimu kwa umma, kwa upande wa sekta binafsi utafiti ulionesha kwamba bado mpango huo hauna nguvu ya kutumia vyombo vya habari kwa ajili ya kutoa habari na kuleta mabadiliko ya mazingira bora ya biashara.
Hali hiyo imechangia matokeo ya awali ya utafiti 2008,Tasisi ya BEST AC kuanzisha mpango wa kusaidia sekta binasfi kushirikiana na vyombo vya habari kwa ukaribu zaidi.
Serengeti Advisers walitoa muongozo kwa ajili ya uchambuzi wa gazeti linaloandika habari zenye viwango kwa ajili ya kusaidia kuusanyaji wa ripoti ya mwaka kwa magazeti yanayoandika mazingira bora ya biashara kwa Taasisi ya BEST-AC .
Repoti ya uchambuzi wa uandishi wa habari za biashara kwa mwaka 2012 ipo katika mtandao ambapo inaonesha matokeo ya utafiti uliofanywa.
Pia hatari ya vyombo vya habari kuandika habari na kuegemea upande mmoja wa habari.
Maadili ya uandishi wa habari yanaeleza kuwa vyombo vya habari vina wajibu wa kutoa habari zenye usahii,na kuiachia umma kutoa maoni yake.
Kushindwa kufanya hivyo kunaweza kuchangia umma kutokuwa na imani kutokana na mfumo wa utoaji habari, hatari iliyopo umma utafuata kile ambacho kilichoandikwa na kinaegemea upande.
Hali ya ongezeko la habari ambazo zinaege upande moja kwa vyombo vya habari inachangia msingi mbaya wa biashara.
Utafiti umegundua kuwa kuna ongezeko uandikaji wa habari za biashara bila kuwa na usawa hali inayochangia uandishi wa habari za biashara kwa magazeti ya Kiswahili kuwa mdogo.
Hamna usawa katika upangaji wa habari za biashara, kuna ubaguzi katika matumizi ya majina na vyeo, kuna ubaguzi katika kuandika takwimu,ubaguzi katika kuvibana vyanzo vya habari,upendeleo katika kuchangua maneno
Taasisi ya BEST-AC ilifanya mkutano na wadau wa masuala ya habai kwa ajili ya kutoa kasoro hizo Januari 17/ 2013.
Mkutano ulijadili ubora wa uandishi wa habari za biashara kwa magazeti.Mkutano huo pia ulikubaliana kuboresha ubora wa habari kutokana na utafiti uliyofanywa 2012 kwa magazeti ya Kiswahili na Kiingereza na uhitaji ni mkubwa.
Wahariri walikuwa na maoni mbalimbali ya nini kifanyike ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri, mafunzo kwa waandishi wa habari za biashara kwa lengo la kupata waandishi wenye viwango vya kuandika habari za Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment