05 February 2013

CHAWATA yaendesha mafunzo kwa walemavu Muheza



Na Steven William,Muheza

CHAMA cha Walemavu wilayani Muheza (CHAWATA)kimeanza semina ya walemavu ya siku tatu wilayani humo ili kuwajengea uwelewa kujua haki zao za kimsingi kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Hayo yalisemwa jana na mwenyekiti wa CHAWATA, Sophia Kassim wakati akizungumza na waandishi wa habari na kubainisha kuwa mafunzo hayo yamefadhiliwa na The Foundation For Civil Society.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo viongozi wa walemavu na wanachama juu ya uwelewa wa kujua haki na wajibu wao katika kukabiliana na changamoto za maisha zilizopo.

Alisema mikakati ya baadae ya chama hicho ni kukabiliana na unyanyapaa dhidi ya walemavu na kuhusiana hasa katika suala la ajira.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa mikakati mingine ni kuwepo miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu, elimu ya Afya kwani walemavu wengi wanakosa elimu hiyo kutokana na kukosekana kwa vitendea kazi

Alisema mafunzo hayo yatafungua ukurasa mpya kwa walemavu kuweza kujitambua na kukabiliana na changamoto zilizopo huku wakiiomba Serikali kuwekeza katika kulisaidia kundi hilo kwani nalo lina mchango katika maendeleo ya Taifa.

No comments:

Post a Comment