01 February 2013

Azam yatamba kuendeleza vipigo


Na Shufaa Lyimo

KLABU ya Azam FC, umesema utaendeleza kipigo katika mchezo wa Ligi Kuu, dhidi ya Mtibwa Sugar.

Azam juzi iliinyuka Toto Africa ya Mwanza mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu mzunguko wa pili, iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jafari Iddi alisema kinachoifanya timu yake ifanye vizuri ni mshikamano uliopo, kati ya wachezaji na viongozi.

"Timu yetu itaendelea kufanya vizuri michezo yote na tunaahidi kuipa kipigo Mtibwa tutakapokutana," alisema.

Hata hivyo alisema ligi ya mwaka huu, ina ushindani mkubwa kwa kuwa kila timu imejipanga kupata ubingwa.

"Ligi hii kwa kweli ni ngumu kwani timu zote zimejiandaa kwa muda mrefu na kila moja, inataka ushindi," alisema.

Aliwataka mashabiki wao kuendelea kuwapa sapoti kila wanapocheza, ili waweze kufanya vyema na kupata matokeo mazuri.

Katika msimamo wa ligi, timu hiyo inakamata nafasi ya pili nyuma ya Yanga, inayoongoza.

No comments:

Post a Comment