31 January 2013

Serikali yashangazwa wageni kufavamia mbunga


Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imeshangazwa na hatua ya wageni kuvamia mbuga mbalimbali na misitu nchini kiasi cha kufanya kuongezeka vitendo vya ujangili na kuahidi kuchukua hatua kali ili kutokomeza ujangili huo.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu. Alisema ili kudhibiti hali hiyo hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa ikiwamo kuimarisha ulinzi katika hifadhi na mapori mbalimbali  ambayo mengine yameanza kutumika vibaya.

Akizungumza mjini Bariadi baada ya kuwaona askari wa kijereshi walioko mahabusu kwa kutuhumiwa kuua majangili, Nyalandu alisema kuwa askari waliopo ni wachache kiasi cha kufanya majangili wengi kuvamia hifadhi na kuua wanyama hususan tembo.

“Kinachosikitisha ni kuwa hawa majangili wamebadilika zamani walikuwa wanawinda kwa ajili ya kupata kitoweo lakini sasa wamebadilika na wanavamia kwa silaha za kijeshi na kuua wanyama bila woga” alisema.

Nyalandu aliahidi kuwa kwa sasa hali hiyo imekuwa kama janga la kitaifa na hivyo kutaka wananchi kubadilika na kukabiliana na majangili ili kulinda maliasili kwa ajili ya vizazi vijavyo.

“Tunahitaji kuajiri vijana wengi kadri inavyowezekana ili kukabiliana na wimbi hili, tunahitaji zaidi ya askari 4,000 na kuanzia mwaka huu tumepewa kibakli cha kuajili vijana 400 ambao tutawasambaza katiak hifadhi na mbuga nyingine," alisema.

Alisisitiza kuwa kwa sasa askari hao wanalinda zaidi ya kilometa za maraba 169 wakati zinazotakiwa ni kilometa za mraba 25 na hivyo kutoa mwanya kwa majangili kuingi na kutoka. Alisema Serikali imeshangazwa na haua ya wageni kuwavamia mbuga mbalimbali na  misitu nchini kiasi cha kufanya kuongezeka vitendo vya ujangili na kuahidi  kuchukua hatua kali ili kutokomeza ujangili huo.

Nyalandu alisema ili kudhibiti hali  hiyo hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa ikiwamo na kuimarisha ulinzi  katika hifadhi na mapori mbalimbali  ambayo mengine.

Akizungumza mjini Bariadi baada ya kuwaona askari wa Kijereshi walioko mahabusu kwa kutuhumiwa kuua majangili, Nyalandu alisema kuwa askari wakliopo ni wachache kiasi cha kufanya majangili wengi kuvamia hifadhi na kuua wanyama hususan tembo.

“Kinachosikitisha ni kuwa hawa majangili wamebadilika zamani walikuwa wanawinda kwa ajili ya kupata kitoweo lakini sasa wamebadilika na wanavamia kwa silaha za kijeshi na kuua wanyama bila woga” alisema.

Nyalandu aliahidi kuwa kwa sasa hali hiyo imekuwa kama janga la kitaifa na hivyo kutaka wananchi kubadilika na kukabiliana na majangili ili kulinda maliasili kwa ajili ya vizazi vijavyo.

“Tnahitaji kuajili vijana wengi kadri inavyowezekana ili kukabiliana na wimbi hili,  tunahitaji zaidi ya askari 4,000 na kuanzia mwaka huu tumepewa kibali cha kuajili vijana 400 ambao tutawasambaza katiak hifadhi na mbuga nyingine.

Alisisitiza kuwa kwa sasa askari hao wanalinda zaidi ya kilometa za maraba 169 wakati zinazotakiwa ni kilometa za mraba 25 na hivyo kutoa mwanya kwa majangili kuingina na kutoka bila ya kupatikana.

Nyalandu alisema nchi ilitarajiwa kuwa na tembo 400,000 mwaka huu  miaka 50 iliyopita na lakini kutokana na kukithiri vitendo vya ujangili wamebakia tembo 110,000 tu  kitu kinachotishia uwepo wa wanyama hao.

No comments:

Post a Comment