31 January 2013

Msanii Bluestar kuachia Tunachafua


Na Queen lema, Arusha

MSANII wa jijini Arusha anayekuja kwa kasi katika muziki wa kizazi kipya,
Hamisi Omari (20) 'Bluestar' anatarajia kuachia singo yake ya tatu inayokwenda kwa jina la Tunachafua.


Akizungumza na gazeti hili jijini hapa juzi, msanii huyo alisema wimbo huo ambao amewashirikisha, Mr Blue na Swaga Boy ameurekodiwa katika studio ya Danlumark ya jijini Dar es

Alisema wimbo huo, utaanza kusikika wiki hii katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni.

“Nawataka wapenzi wa muziki wa kizazi kipya na mashabiki wangu kwa
ujumla, wakae mkao wa kula kupokea wimbo huo kwani ni moto wa kuotea
mbali,” alisema Bluestar.

Alizitaja nyimbo zake nyingine alizozitoa mwaka jana ni Digidagi aliyemshirikisha Chris G na Njoo.

Msaanii huyo ambaye alianza muziki mwaka jana, alisema lengo
lake ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa.

Alisema anatarajia kutoa albamu yake ya kwanza katikati ya mwaka huu, ambapo amewataka mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kumuunga mkono.

No comments:

Post a Comment