29 January 2013

Kisandu amtega Zitto


Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Uhusiano na Uenezi Taifa, Kitendo cha Vijana wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. Deogratius Kisandu, amesema Tanzania imekosa vijana wazalendo ndio sababu ya kushindwa kutekeleza wanachokisema.


Bw. Kisandu aliyasema hayo katika taarifa yake aliyoitoa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), kushindwa kuwataja vigogo walioweka mabilioni ya fedha nchini Uswisi.

Alisema kitendo cha Bw. Kabwe kushindwa kuwataka vigogo hao ni kuwahujumu Watanzania ambao walitegemea angewataja ili kuonesha uzalendo badala yake suala hilo ameiachia Serikali.

“Serikali haiwezi kuwataja vigogo husika, Bw, Kabwe alipaswa kuonesha uzalendo wa kuwataka kama kweli ana uhakika, hakuna haja ya kusubiri upelelezi au kuundwa kamati wakati tayari alishasema majina yao anayo,” alisema Bw. Kisandu.

Aliongeza kuwa, umefika wakati wa Wanasiasa waache kuwahadaa wananchi bali wawe wawazi na wenye uchungu na Taifa lao hasa ukizingatia kuwa, walimu wanalia mishara midogo na wajasiliamali kukosa mikopo ya mabilioni ya Rais Jakaya Kikwete.

Alisema Mtwara wanalia njaa hivyo kugomea gesi isitoke nje ya Mkoa huo wakati kuna fedha nyingi ambazo zingeweza kuokoa
maisha ya Watanzania.

“Serikali haihitaji kuunda kamati wala tume bali wahusika watajwe moja kwa moja...kama Bw. Kabwe atashindwa kuwataja mimi nipo taayari kuwataja Februari mwaka huu kama atanipa majina hayo.

“Wakati wa kuogopana umekwisha, hivi sasa tunajenga Taifa na kama atashindwa kufanya hivyo ni bora avuliwe ubunge maana hajawatendea haki Watanzania..hatuhitaji viongozi ambao wanashindwa kutekeleza walichokisema,” alisema.


No comments:

Post a Comment