29 January 2013

BoT yataka Katiba Mpya iwabane wanasiasa wasiingilie utendaji

Anneth Kagenda na Rehema Maigala

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imependekeza kuwekwa kipengele cha sheria ambacho kitawabana wanasiasa kutoingilia kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na benki hiyo.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndullu, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa maoni ya Katiba Mpya kwa tume inayoratibu mchakato huo.

Alisema BoT ina jukumu la kutoa huduma nyeti za kiuchumi kwa wananchi wake hivyo haitakiwi kuingiliwa na mambo ya kisiasa.

“Utendaji kazi wa BoT usiingiliwe na siasa kwani ina mambo muhimu ya kufanya ili kukuza uchumi katika Taifa letu hivyo
ipewe uhuru wa kufanyakazi,” alisema.

Aliongeza kuwa, pia kuwepo na sheria mama kwenye Bunge za kuikinga BoT kufanya mambo yake yenyewe bila kuingiliwa ambapo kwa kufanya hivyo kutaboresha utendaji kazi wake.

Akijibu maswali ya waandishi likiwemo la watu kuficha fedha nje ya nchi, Prof. Ndullu alisema historia inaonesha kuwa, watu waliokuwa na fedha nyingi walikuwa wakipeleka fedha zao
nje ya nchi tofauti na sasa ambapo watu wachache wanaiba
fedha na kwenda kuzificha nje.

“Hvi sasa watu wanaiamini nchi yao na fedha nyingi wanazihifadhi nchini...kwa mfano, fedha ya haraka ninayoweza kusema iko nchini ni dola za Marekani bilioni 2.2 hatujahesabu na zingine zilizopo nje hivyo ninachoweza kusema ni kwamba, watu wamewekeza sana kwenye nchi yao na wameiamini,” alisema Prof. Ndullu.

Akizungumzia suala la kutakatisha fedha, Prof. Ndullu alisema ni vigumu kulizungumzia lakini anaamini kama Katiba Mpya itaweka sheria anazozisema, zitaweza kuainisha jambo hilo.

2 comments:

  1. Ndulu bwana, sheria zipo tatizo uenda kutojiamini kwako na wenzio waliopita kutoa bwana wa Chadema. Mnaogopa kupoteza kitumbua ndio maana mnatumika na wanasiasa. Haiwezekani, ufanye unavyotaka lazima uwe chini ya chombo cha kukuthibiti. Dhamila yako ya kwenda pale ndio dawa lakini kama kupata ajira BOT inakushinda. CB gani haiwezi to control inflation ni BOT tu. Tatizo, Ndullu. Achia ngazi kwani umetamka unatumika.

    ReplyDelete
  2. SINA UHAKIKA HILI BUNGE LA MAKABWELA [HOUSE OF COMMON] LITAKUWA NA MADARAKA LILIYO NAYO NI MATUMAINI YETU YATAKUWEPO MABUNGE MENGINE SAMBAMBA [HOUSE OF SENATE]BUNGE LA MARAIS WASTAAFU NA [HOUSE OF LORDS]BUNGE LA MABWANYENYE

    ReplyDelete