30 November 2012

UBADHIRIFU WA BILIONI 86/- Mnyika ambana William Ngeleja *Adai wizi huo ulitokea akiwa Waziri wa Nishati *Amtaka Muhongo asiwe muoga wa kujibu hoja


Na Daud Magesa, Mwanza

MBUNGE wa Ubungo Bw. John Mnyika, amesema aliyekuwa Waziri wa Nishati, Bw. William Ngeleja, hawezi kukwepa ukiukwaji wa sheria katika manunuzi ya mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura.

MAZISHI

Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Kissa Gwalugano Mohamed,ambaye ni mke wa Mbunge wa Wawi,Zanzibar Bw.Hamad Rashid Mohamed,kwenda msikitini na mazishi kufanyika jana jioni katika makaburi ya Kisutu,Dar es salaam.

Maalim Seif aongoza mamia kumzika mke wa Hamad Dar


Na Goodluck Hongo

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, jana aliongoza mamio ya waombelezaji katika mazishi
ya Kissa Gwalugano Mohamed ambaye ni mke wa Mbunge wa
Wazi, Zanzibar Bw. Hamad Rashid Mohamed.

KATAZO



Pamoja na kuwapo kwa alama za usalama barabarani (kulia juu) inayokataza kuegeshwa kwa vyombo vya moto kando ya Barabara ya Bagamoyo eneo la Sayansi, Kijitonyama Dar es Salaam, baadhi ya waendesha bajaj wanapuuza agizo hilo kwa kuegesha katika eneo hilo, Kama walivyokutwa jana (Picha na Charles Lucas)

Mapigano Tegeta mmoja ajeruhiwa shavu la kushoto


Na Angelina Faustine

MKAZI wa Tabata, Bw. John Paulo (20), jana alipata majeraha katika shavu la kushoto wakati polisi walipopiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi katika eneo la Tegeta.

UZINDUZI


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, akifungua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za kisasa eneo la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Bw. James Lembeli na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdulkarim Shah. (Picha na Charles Lucas)

Majambazi 10 wakamatwa Dar *Wakutwa na SMG, gari, simu ya upepo


Na Angelina Faustine

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia majambazi sugu 10, waliokamatwa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam na Pwani wakiwa na silaha mbalimbali za moto walizokuwa wakizitumia kufanya uhalifu na mauaji.

MAUA


Baadhi ya wafanyabiashara wa maua wakipanga bidhaa hizo juu ya uzio wa bati zilizozungushiwa katika nyumba inayojengwa Mtaa wa Agrey Kariakoo, kama walivyokutwa na mpigapicha wetu, Dar es Salaam jana. Kufanyabiashara katika eneo la shughuli za ujenzi unaweza kuhatarisha maisha yao na wateja. (Picha na Prona Mumwi)

BAKWATA waanza kutoa ushahidi kesi ya Ponda



Na Rehema Mohamed

KESI ya kuvamia uwanja wa Markas inayomkabili Shekhe
Ponda Issa Ponda na wenzake 49, imeanza kuunguruma jana.

MATUNDA


Mfanyabiashara wa matunda akiwauzia wateja bidhaa hiyo katika eneo la Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana. Ufungaji wa matunda yaliyomenywa katika pakiti uboresha huduma hiyo. (Picha na Heri Shaaban)

Ole Naiko apewa tuzo ya utumishi bora serikalini


Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji mstaafu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Emmanuel Ole Naiko, amepewa tuzo ya ushindi wa kwanza ya utumishi bora wa umma kutokana na juhudi zake
za kusaidia ukuaji wa sekta binafsi nchini.

TUZO


Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikali kwenye Kampuni binafsi ya African Barrick Gold (ABG), Bw. Emmanuel Ole Naiko (kushoto), akipokea tuzo ya ushindi wa kwanza ya utumishi bora wa umma kutokana na juhudi zake
za kusaidia ukuaji wa sekta binafsi nchini. Kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni binafsi nchini, Bw. Ali Mufuruki, Dar es Salaam juzi.
(Na Mpigapicha wetu)

Tumetumia dola milioni 100 kusaidia maendeleo -Shirika


Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Plan International, limetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 100, katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili.

Avunjika mguu, mbwa akimbia na mfupa wake



Na Thomas Kiani, Singida

MKAZI wa Mtaa wa Murumba, Kijiji cha Munyu, Kata ya Irisya, Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, Bw. Yahaya Jumanne (30), amevunjika mguu wa kushoto baada ya kupata ajali ya pikipiki
na mfupa wake kuokotwa na mbwa.

MAONESHO


Rais wa Shirikisho la Maonesho ya Kimataifa la Meridyen ya Uturuki, Bw. Oguz Yalcin, akimkabidhi Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda, kitabu cha  mwaliko wa kushiriki maonesho yatakayofanyika nchini humo hivi karibuni, mara baada ya kutembelea maonesho katika  Viwanja vya Maonesho vya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere Sabasaba, Dar es Salaam jana. (Picha na Prona Mumwi)

Tuwasaidie yatima kielimu, kuboresha maisha yao



KITANDA usichokilalia, huwezi kujua kunguni wake, shida na mateso wanayopata watoto waishio katika mazingira hatarishi na wale wa mitaani ni vigumu kuelezea.

29 November 2012

WAWEKEZAJI


Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza (wa pili kulia), akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Gwata, mkoani Pwani, wakati wakati wa kuwatambulisha wawekezaji watarajiwa wa kilimo cha mpunga na miwa ambao watatumia treni ya TAZARA, (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Raymond Mbilinyi, Kulia ni Meneja wa Mkoa wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Mhandisi Abdallah Shekimweri. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya SAGCOT, Bw. Godfrey Kirenga. (Picha na Charles Lucas)

Hamad Rashid akwaa kisiki mahakamani,Pia apata msiba wa mkewe

Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana ailishindwa kutoa uwamuzi wa kesi ya Mbunge wa Wawi Zanzibar, Bw.Hamadi Rashid na wenzake 10 dhidi ya Wadhamini wa CUF, kutokana na uwamuzi huo kutokamilika kuandaliwa.

MSHINDI ZUKU


Mshindi wa tatu wa shindano la 'Shinda Biashara na Mtaji' kutoka ZUKU Bw. Muhaji Hassan (kushoto) mkazi wa Zanzibar akipeana mkono na Meneja  Biashara wa gazeti hili, Bw. Cecil Mushi, wakati wa makabidhiano ya zawadi za ving'amuzi na madishi kwa washindi, Dar es Salaam jana, (wa kwanza kulia) ni Msanifu Mkuu wa Habari wa gazeti hili, Bw. Samwel Petro na judith Kereth wa Idara ya Usambazaji. (Picha na Anna Titus)

Vodacom yazindua duka la mauzo Dar



Na Darlin Said

KAMPUNI ya Vodacom imezindua duka jipya la mauzo ambalo litasaidia kupunguza msongamano wa wateja kwenye maduka mengine.

Uzinduzi huo uliofanyika Dar es Salaam jana ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rubenanga .

TBS, wadau wajadili viwango lisha ya watoto


Na Rachel Balama

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS)na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na lishe nchini wamekutana kujadili viwango saba katika lishe na chakula kwa ajili ya matumizi maalum ya watoto vitakavyotumika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

VETA yaanika madhara ya ukosefu wa mitaji



Na Willbroad Mathias

TATIZO la ukosefu wa mitaji kwa vijana wanaohitimu Vyuo vya Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA) limeelezwa kuwa ndicho chanzo cha vijana hao kushindwa kujiajiri.

Tanzania yapongezwa kutoa elimu ya chanjo


Na Jesca Kileo

TANZANIA imepongezwa kwa matumizi mazuri ya chanjo na elimu wanayoitoa kwa wanawake kuhusu umuhimu wa chanjo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wao wenyewe.

MAZISHI

Vijana wakiwa wamepanda  mnazi kuona mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashirb Nkoromo).


Serikali yatoa kauli nzito *Simanzi vilio vyatawala msibani




Na Benedict Kaguo,Muheza

SERIKALI wilayani Muheza imetoa muda wa saa 24 vinginevyo italazimika kutumia nguvu ya dola kuwasaka na kuwafikisha mahakamani wananchi wote wa Kijiji cha Songa Kibao Maguzoni waliohusika na wizi
wa mali za Msanii Hussein Ramadhan Mkieti 'Sharo Milionea', aliyezikwa jana Lusanga Muheza.

Kili Stars yakwaa kisiki Namboole


Na Mwandishi Wetu, Kampala

TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), jana ilikwaa kisiki baada ya kufungwa bao 1-0 na Burundi katika mechi ya michuano ya Chalenji iliyochezwa Uwanja wa Mandela.

UZIDUZI


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Rugimbana, akikata utepe wakati wa ufunguzi wa duka jipya la Huduma kwa Wateja wa Vodacom, Dar es Salaam jana, lililopo Barabara ya Haile Selasie Oysterbay, duka hilo linatarajiwa kupunguza msongamano wa wateja. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza na Meneja wa Duka hilo, Bi. Lilian Kimaro. (Picha na Anna Titus)

SUMATRA yapokea maoni ongezeko la nauli



Na Leah Daudi

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini(SUMATRA),imepokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu mapendekezo ya ongezeko la nauli kwa mabasi yaendayo mikoani.

Serikali yaombwa kusimamia mfumuko wa bei za vyakula


Na Rose Itono

WANANCHI wameiomba serikali kusimamia bei za bidhaa ili kuwapunguzia mzigo mkubwa wananchi kutokana na kupanda kwa bei kiholela.

28 November 2012

SALAMU

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia), akisalimiana na Shekhe Mkuu wa Bagamoyo, mkoani Pwani, Abdallah Masoud Jembe, anayesumbuliwa na maradhi alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Ramiah, mjini humo. Picha na OMR

Jerry Muro kortini tena *Kesi aliyoshinda kusikilizwa upya Mahakama Kuu



Na Rehema  Mohamed

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa
kuanza kusikiliza rufaa ya Serikali dhidi ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC1), Bw. Jerry Muro na wenzake.

Wakazi wa Dar wakamatwa na dawa za kulevya Z'bar


Na Mohammed Mhina, Jeshi la Polisi Zanzibar

WAFANYABIASHARA wawili wakazi wa Dar es Salaam, wametiwa mbaroni visiwani Zanzibar baada ya kukamatwa wakiingiza dawa za kulevya kwa njia ya majini.

Mnyika aivaa serikali, wabunge CCM


Na Daud Magesa, Mwanza

MBUNGE wa Ubungo, Bw. John Mnyika, amesema umaskini uliopo nchini umetokana na udhaifu wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wabunge wa chama hicho.

UMEME


Mkazi wa Dar es Salaam akipita kando ya mashine za kufua umeme (Generator) kama zilivyo kutwa nje ya maduka kwenye Mtaa wa Agrey, Kariakoo jana. Tatizo la kukatika umeme linasababisha kuongezeka kwa matumizi ya mashine hizo. (Picha na Prona Mumwi)


DC awabana vigogo wa serikali *Aagiza wanyang'anywe ardhi waliyopewa


Na Yusuph Mussa, Korogwe

MKUU wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Bw. Mrisho Gambo, ameagiza vigogo wote wa Serikali waliopewa ardhi kinyembela kwenye Kata ya Mswaha-Darajani, Tarafa ya
Mombo, wanyang’anywe akiwemo Bw. Jonas Malorsa
(aliyekuwa Mweka Hazina wa Halmashauri Wilaya ya
Korogwe), ambaye hivi sasa amesimamishwa kazi.

Vigogo wa TAZARA wapewa dhamana



Na Rehema Mohamed

MHANDISI Mkuu na Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Reli
ya Tanzania na Zambia (TAZARA), ambao juzi walifikishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakikabiliwa na tuhuma za kutumia madaraka vibaya
na kuisababishia Serikali hasara ya sh. milioni 120, jana
wamepewa dhamana baada ya kutimiza masharti.

KATUNI


Abood lapata ajali, lajeruhi wanafunzi 7



Rehema Maigala na Rose Itono

WANAFUNZI saba wa Shule ya Awali ya Mount Moria, iliyopo Kibamba, Dar es Salaam, wamejeruhiwa baada ya basi la shule walilokuwa wamepanda kugongwa na basi la Kampuni ya Abood, ambalo lilikuawa likitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Watu wenye ulemavu wapewe fursa ya ajira



Desemba 31 kila mwaka, Tanzania ni miongoni mwa nchi mbalimbali duniani zinazoadhimisha siku ya watu wenye
ulemavu.

MSAADA


Mkurugenzi Mkazi wa Plan Internatinal, Bw. David Muthungu, akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, kuhusu mpango wa taasisi hiyo ya Kimataifa wa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi nchini. Kulia Ofisa Mtendaji Mkuu, Bw. Nigel Chapman. (Picha na Peter Twite)

Wizara yawapeleka wakulima 14 katika maonesho ya kilimo Sudan



Na Mariam Mziwanda

WIZARA ya Kilimo, Chakula na Ushirika, imewagharamia wakulima kutoka mikoa tisa nchini kwenda nchini Sudan ili
kushiriki maonesho ya kilimo.

Mbunge CCM alalamika kupigwa vita


Na Yusuph Mussa, Korogwe

MBUNGE wa Korogwe Vijijini, mkoani Tanga, Bw. Stephen Ngonyani (CCM), amesema baadhi ya wanachama wanzake
wanampiga vita kwa kukataa kutangaza miradi anayoipeleka
katika kata zao.

TAMKO URANI


Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (HLRC), ambaye pia ni Mwanasheria kituo hicho, Bi. Imelda Urio, akitoa tamko mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, kuitaka Seriakali kusimamishi uchimbaji wa madini ya urani kuepuka madhara kwa wananchi. Kushoto ni Mchungaji John Magafu. (Picha na Charles Lucas)

27 November 2012

Serikali mtegoni waliofuja bil. 86/- *Mnyika aahidi 'kuwaanika' wahusika *Adai ni sehemu ya ufisadi mkubwa


Na Eckland Mwaffisi

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika, amesema wizi wa sh. bilioni 86, unaodaiwa kufanywa na watumishi wa Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ni sehemu ya ufisadi mkubwa katika utekelezaji wa Mpango wa Serikali wa kufua umeme wa dharura.

Nchi 48 zawekwa kundi la nchi maskini duniani


Na Rachel Balama

UMOJA wa Mataifa (UN), umeziweka nchi 48 katika kundi la nchi maskini duniani (LDCs), zikiwemo nchi 33 za Afrika, Asia (9), Pacific (5) na Caribbean (1).

JK awaapisha Majaji, Katibu Tume ya Sheria


Na Grace Ndossa

RAIS Jakaya Kikwete, jana amewaapisha Majaji wawili wa Mahakama ya Rufaa, mjumbe wa Tume ya Uchaguzi na
Katibu wa kurekebisha sheria.

Mvua za El-nino 'zayeyuka'



Na Stella Aron

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imewahadharisha i wananchi kutumia maji kwa uangalifu na kuhifadhi malisho kwa ajili ya mifugo kutokana na mvua ndogo zilizonyesha hadi sasa.

BTL, Levi Electronics wakabidhi zawadi kwa washindi wa ZUKU


Na Peter Mwenda

KAMPUNI ya Business Times Limited (BTL), kupitia gazeti lake la Majira kwa kushirikiana na Kampuni ya Wananchi, kupitia wakala wake Levi Electronics anayesambaza bidhaa ya ZUKU TV, jana wamekabidhi zawadi ya ving'amuzi na dish kwa washindi wawili
kati ya watatu wa shindano la “Shinda Biashara na Mtaji”.

UGOMVI


Mwendesha GUTA akidhibitiwa na mtembea kwa miguu (kushoto) ili asitoroke, baada ya kumgonga kwenye Barabara ya Msimbazi, Kariakoo Dar es Salaam jana. (Picha na Peter Twite)

Kortini wakidaiwa kuisababishia serikali hasara



Na Rose Itono

MHANDISI Mkuu wa Mitambo na Meneja wa Fedha wa Shirika
la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kujibu mashtaka mawili likiwemo la kuisababishia Serikali hasara
ya sh. milioni 120.

Polisi kufanya mandamana ya kupinga ukatili wa kijinsia


Jesca Kileo na David John

JESHI la Polisi nchini, leo litafanya maandamano ya kwanza tangu lianzishwe ili kupinga ukatili wa kijinsi kwa watoto na wanawake.

Akosa sh. 7,700 kwa kushindwa kumaliza ndizi 70, akwamia 40


Na  Patrick Mabula, Kahama

KATIKA hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Mjini Kahama, mkoani Shinyanga, Bw. Seleman Hamis (27), juzi aliwashangaza wakazi
wa huo baada ya kutamba kumaliza ndizi mbivu 77 lakini alipofika ya 40, alichemsha na kujikuta katika wakati mgumu.

KAMARI


Askari wa Manispaa ya Ilala wakiondoa banda linalotumika kuchezesha kamari bila kibari, kwenye makutano ya Mitaa ya Kipata na Msimbazi, Kariakoo Dar es Salaam jana. (Picha na Peter Twite)

Wassira awataka viongozi CCM kutatua matatizo ya wananchi


Na Raphael Okello, Bunda

MBUNGE wa Bunda, mkoani Mara, Bw. Stephen Wassira, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimefanya kazi
kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo lakini bado
kinakabiliwa na matatizo mbalimbali.

Wanaume watano mbaroni wakidaiwa kuuza miili yao


Zubeda Mazunde na Angelina Faustine

JESHI la Polisi mkoani Ilala, linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kufanya biashara ya kuuza miili yao.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Marietha Komba, alisema watu hao walikamatwa juzi, saa tano asubuhi katika eneo ya Buguruni Chama, jijini Dar es Salaam.

Watu watatu wafariki katika matukio tofauti



Na Lilian Justice, Morogoro

WATU watatu wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani Morogoro, likiwemo la mwanafunzi wa darasa la saba katika
shule ya Msingi Maguha, iliyopo wilayani Kilosa, Rina Gidion
(7), kugongwa na gari.

WASTAAFU


Waliokuwa wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Kitengo cha Ufundi Reli mkoani Kigoma kabla ya kuvunjika jumuiya hiyo mwaka 1977, Bw. Hamisi Ramadhani na Fundi Rashid (kushoto) wakiwa katika makazi ya muda kwa miaka miwili eneo la Stesheni, Dar es Salaam jana,  wakati wakisubiri kulipwa na Serikali stahili zao. (Picha na Charles Lucas)

26 November 2012

Wana mazingira mko wapi mbona nchi inateketea?



Na Michael Sarungi

TAKWIMU zilizopo zinaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambayo kila ifikapo Juni 5 ya kila mwaka, huadhimisha siku ya mazingira.

MARUNDO YA MAGOGO

Uchomaji wa mkaa ni moja ya sababu zinazochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira,kama inavyoonekana pichani rundo la magogo likiwa limetayarishwa tayari kwa ajili hiyo

Ziko wapi benki zitazowakomboa maskini?


Na Michael Sarungi

NI lini tutakuwa na benki zitakazoungana na  taasisi nyingine za fedha kwa ajili ya kupambana na umaskini unaowatesa Watanzania kwa muda mrefu?

MBOGAMBOGA

Aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu wa Viwanda na Biashara, Bw. Lazaro Nyalandu akiangalia mbogamboga alipotembelea soko la Tandale

Makene Juma Chipukizi wa Hoilers mwenye ndoto za kucheza NBA


Na Victor Mkumbo

KATIKA sanaa mbalimbali ikiwa ni pamoja michezo ya aina tofauti, kumekuwa na vipaji lukuki ambavyo vinajitokeza kila siku.

HIFADHI YA SAANANE

Tembo wakiwa katika Hifadhi ya Saanane

Hifadhi ya Saanane kivutio cha watalii ndani na nje


Na Jovin Mihambi

MOJAWAPO ya shughuli za serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ni kuendeleza sekta ya utalii wa ndani na nje ili kuweza kuliongezea Taifa pato kubwa linalotokana na sekta ya utalii.

Umakini wa Zitto tumaini la Taifa


Na Gladness Mboma

BWANA Zitto Kambwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini ni Mwanasiasa aliyechipukia katika duru ya siasa nchini, kwa kutoa hoja zenye ukweli na serikali kulazimika kuzifanyia kazi,hali hiyo imesababisha aonekane kwamba anafaa katika uongozi wa juu kutokana na kutoa kauli nzito zenye kusaidia Watanzania.

Alichonena Lowassa kinapaswa kufanyiwa kazi


Na Michael Sarungi

KATIKATI ya wiki iliyopita Waziri Mkuu aliyejiuzulu.Bw. Edward Lowasa,alitoa alitoa wito kwa serikali akisema kuwa huu ni wakati muafaka kwa elimu ya sekondari kutolewa bure kama ilivyo elimu ya msingi.

JK AKABIDHIWA CHETI

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhombili,Profesa Ephata Kaaya (Kushoto),akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete,Cheti cha Udaktari wa Afya ya Umma (Honoris Causa),kutokana na Shahada aliyotunukiwa na chuo hicho Desemba 2012,kwa kutambua mchango wake wa kuendeleza sekta ya afya nchini.Picha na Ikulu

Vigogo BoT walipa faini kukwepa kifungo



Na Rehema Mohamed

MAOFISA watatu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao juzi walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh. milioni 5 kila mmoja, jana wameachiwa huru baada ya kutimiza sharti la kulipa kiasi hicho cha fedha.

TIBA ASILI


Wanawake wa kimasai wakitoa huduma ya tiba asili eneo la Magomeni, Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmoja wa wateja akisikiliza kwa makini ushauri wa tiba hiyo. Kupanda kwa fghalama za matibabu hospitalini kunasababisha baadhi ya watu kukimbilia huduma za dawa asili. (Picha na Charles Lucas)

JK apokea taarifa ya maendeleo ujenzi wa kampasi tiba za afya


Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete, jana amepokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kampasi mbili za tiba ya afya zinavyojengwa katika
Chuo Kikuu cha Dodoma na Mloganzila huko Kisarawe,
ambazo pia zitatumika kama hospitali.

Urais 2015 CHADEMA moto *Zitto aanika msimamo wake, atoa neno


Na Rehema Maigala

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema kama chama chake hakitampa ridhaa ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu 2015, ataachana na ubunge.

USAFI


Mkazi wa jiji akisafisha daladala lililokuwa katika foleni ya kupakia abiria, kama alivyokutwa Shule ya Uhuru Barabara ya Msimbazi, Dar es Salaam jana. Uoshaji huo unatokana kukosa muda wa kuyapeleka katika maeneo maalumu ya kuoshea. (Picha na Charles Lucas)

Polisi Dar wakamata majambazi sugu watano


Zubeda Mazunde na Angelina Faustine

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewakamata majambazi sugu watano wakiwa na silaha mbalimbali za moto walizokuwa wakizitumia kufanya matukio ya uhalifu na mauaji.

CCM wataka M/kiti Chadema aburutwe kortini



Na Mwandishi Wetu, Geita

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Katoro Mazemule, mkoani Geita na wenzake wanaodaiwa kuhusika na wizi wa sh. milioni 16.5 za halmashauri
ya kijiji hicho, wafikishwe mahakamani haraka.

MSAJILI MAHAKAMA KANDA YA ZIWA AOMBA FAIRI KULICHUNGUZA


Na Timothy Itembe Tarime

MSAJILI wa Wilaya Mahakama kuu ya kanda ya ziwa Mwanza Tanzania ameitisha fairi
kesi No 57/2010 na No 7/2012 baina ya mdaiwa Mugore Mang'u na mdai Peter Zackaria
Kiyonge kuchunguza Shauri hilo ili kulitolea mwafaka.

DAMU


Meneja wa Mpango wa Damu Salama Tanzania, Dkt. Efesper Nkya, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu Salama itayofanyika leo kwa Taasisi ya Khoja Shia Ithnasheri. Kushoto ni Mratibu wa taasisi hiyo, Bw. Fazleabbas Dhirani. (Picha na Peter Mwenda)

Wekeni kipaumbele fani ustawi wa jamii-Meya


Na Florah Temba,
Moshi.

SERIKALI imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuweka kipaumbele zaidi kwenye fani ya ustawi wa jamii, hatua ambayo itasaidia kupunguza matatizo yaliyopo katika jamii ikiwemo vitendo vya ukatili dhidi ya
watoto na wanawake.

Acheni kulima karibu na nguzo za umeme-TANESCO


Na  Patrick Mabula,
Kahama

SHIRIKA la Umeme Taznzania (TANESCO) wilayani Kahama limewataka wananchi kuacha kulima karibu na
nguzo za umeme kwa kuwa zinasababisha kuoza na kuanguka

Halmashauri Korogwe yashtakiwa CCM



Na Yusuph Mussa, Korogwe

MKUU wa Wilaya ya Korogwe Bw. Mrisho Gambo ameishitaki Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa inanyanyasa wabeba abiria kwa njia ya pikipiki maarufu kama bodaboda pamoja na mamalishe.

WAZAZI


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdallah  Bulembo, akizungumza na Wafanyakazi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tegeta (hawapo pichani) wakati wa ziara ya siku moja ya kutembelea shule za jumuiya hiyo, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dogo Mbarouk na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Utekelezaji Wazazi Taifa ambaye pia Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Bi. Angela Kiziga. (Na Mpigapicha Wetu)

Wananchi Gezaulole wadaiwa kunywa maji ya kemikali

 Na.Lilian Justice,
 Kilosa.

WANANCHI wanaoishi katika maeneo ya Gezaulole  nyumba namba 30, 38 katika mji mdogo wa Ruaha Wilayani Kilosa  mkoani Morogoro wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi na hivyo kupelekea kunywa maji ya kemikali yatokayo kiwandani.

Bilal kuweka jiwe la msingi nyumba za gharama nafuu NHC


Na Rachel Balama

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi kwenye mradi wa nyumba 94 za makazi za Shirika la Nyumba la  Taifa (NHC) zilizopo katika eneo la Ilembo mjini Mpanda, mkoani Katavi.

Bashe,Membe mgogoro mzito

Na Mariam Mziwanda

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Hussein Bashe ameeleza kuwa kwa maslai mapana ya taifa na chama ataendelea kutetea kauli yake na kusimamia aliyoyasema kwenye mkutano mkuu wa chama hicho mjini Dodoma kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  Bernard Membe ni mtu hatari na mnafiki.

Waganga wa jadi watakiwa kuacha utapeli Njombe


Na Joseph Mwambije

Njombe

WAGANGA wa jadi Nchini wametakiwa kuacha utapeli na
kuwaambia wateja wao ukweli kama matatizo yao yanatakiwa kutibiwa Hospitali na
kuacha kuwadanganya Wateja wao kuwa wamerogwa wakati homa wanazoumwa ni za
kutibiwa Hospitali.

23 November 2012

KATUNI


Thabo Mbeki: Viongozi Wazee chanzo cha umaskini TZ




Na Grace Ndossa

RAIS mstaafu wa Afrika Kusini, Bw. Thabo Mbeki, amesema Tanzania imeshindwa kupiga hatua ya maendeleo kwa sababu ya viongozi wenye umri mkubwa kuendelea kung'ang'ani madaraka.

Nipo tayari kuitumikia CCM kimwili, kiakili


Na Mwandishi Wetu, Rukwa

KATIBU Mkuu wa CCM, Bw. Abdulrahman Kinana, amesema yupo tayari kimwili na kiakili kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ili kuwasidia Watanzania.

HUDUMA YA VODACOM


Mkazi wa Moshi, Felister Raymond (kushoto) akipimwa damu na Dkt. Elibariki Kalua wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), wakati wa kliniki ya upimaji afya bila malipo, uliodhaminiwa na  Vodacom Foundation, uliofanyika katika Viwanja vya Hindu Mandal Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro jana. (Na Mpigapicha Wetu)  

Tanzania kupeleka Wanajeshi DRC *Membe ahuzunishwa na msimamo wa UN



Na Darlin Said

TANZANIA ipo tayari kupeleka wanajeshi 1,000 nchini Congo (DRC), wakaungane na wanajeshi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jeshi la nchi za
Maziwa Makuu ili wakapambane na waasi wa Kundi cha
M23 ambacho kimeuteka mji wa Goma.

NYUNGO


Mchuuzi wa nyungo (jina halikufahamika) akivuka, Barabara ya Chang'ombe wilayani Temeke, Dar es Salaam jana wakati akisaka wateja. Baadhi ya wachuuzi wa bidhaa hizo hulazimika kutembeza mitaani badala ya kujenga vibanda ili kuepuka kukamatwa na askari wa manispaa. (Picha na Peter Twite)

DC Korogwe sasa 'atapika nyongo' kwa wanasiasa



Na Yusuph Mussa, Korogwe

MKUU wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Bw. Mrisho Gambo, jana 'ametapika nyongo' baada ya kuwapasha wanasiasa wilayani humo kuwa hana mpango wa kugombea ubunge wala Uenyekiti wa halmashauri hiyo na kudai kuwa nafasi aliyonayo ni ya kuteuliwa na Rais ambaye ndiye anayeweze kumuondoa.

Alichosema Rais Mbeki ni muhimu kuzingatiwa kwa masilahi ya nchi



RAIS mstaafu wa Afrika Kusini, jana alikutana na viongozi mbalimbali pamoja na wafanyabiashara kujadili changamoto
mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika.

UONGOZI


Baadhi ya viongozi mbalimbali wakisikiliza mada katika kongamano la kujadili masuala ya utawala bora na uongozi kwa nchi za Afrika lililoandaliwa na taasisi ya Kimataifa ya Thabo Mbeki Foundation ya Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki, Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Balozi Dumisani Kumalo wa taasisi hiyo, Balozi wa Afrika ya Kusini nchini, Thanduyise Chiliza na Mwanasheria wa taasisi hiyo, Mojanku Gumbi. (Picha na Charles Lucas)

Mbunge awashawishi wananchi kuwacharaza viboko watendaji


Na Sophia Fundi, Karatu

Mbunge wa Karatu, mkoani Arusha, Mchungaji Israel Natse (CHADEMA), amewataka wananchi kuwacharaza viboko
watendaji wote wanaokaa ofisini badala ya kwenda kwa
wananchi kusikiliza matatizo yanayowakabili.

Dk. Slaa: CCM itekeleza sera ya elimu bure kwa vitendo



Na Livinus Feruzi, Karagwe

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema hakina tatizo na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza sera yao ya elimu bure na kushushwa kwa gharama ya vifaa vya ujenzi ili kuchochea maendeleo ya Watanzania.

ZIARA


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima (kushoto) akisikiliza maelezo ya Kamishina wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Laurence Kabigi, wakati wa ziara ya kukagua shughuli za kikosi hicho, Dar es Salaam juzi. (Picha na Peter Mwenda)

Dkt. Mwakyembe 'aikoromea' Bodi Mpya TPA



Na Mashaka Mhando, Tanga

WAZIRI wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema Wizara hiyo itasaini mkataba wa miezi sita na Bodi ya Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), aliyoichagua hivi karibuni na kama itashindwa kufikia malengo waliyopewa itaondolewa.

'Katiba Mpya ivibane vyama vinavyoshika dola'


Na Mwandishi Wetu, Mara

MKAZI wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, Bw. Marco Magubo (31), amependekeza kuwa Katiba Mpya ikataze vyama vya siasa vinavyoingia madarakani baada ya kushinda Uchaguzi wa Rais, visipeperushe bendera ya chama badala
yake vitumie bendera ya Taifa.

22 November 2012

Wazee watakiwa kukemea vijana kukaa vijiweni






Na Stella Shoo,
Morogoro.

WAZEE wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro wameshauriwa kukemea tabia ya vijana na watoto wao kukaa vijiweni na kunywa pombe bila kujishughulisha na uzalishaji,kwani tabia hiyo haitaweza kutokomeza umaskini unaoikabili jamii wilayani humo.

Vijana watakiwa kujitokeza kutoa maoni ya katiba mpya


Na Jesca Kileo

KATIBU wa Mkoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Vyuo vya Elimu ya Juu, Bw.Christopher Ngubiagai ametaka vijana wasomi wa mkoa huo kutokubali kulishwa maneno na badala yake wajitokeze kwa wingi kutoa maoni juu ya upatinaji wa Katiba Mpya ya Tanzania.

Wanaosema CCM aijafanya chochote hawama jipya


Na Darlin Said

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Mzimuni  Bw.Faraji Ngonyani amewashangaa wale wote wanaosema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakijafanya kazi yeyote na kusema kuwa hawana jipya.

Afariki dunia kwa kujinyonga



Zubeda Mazunde na
Angelina Faustine.

MKAZI wa Ulongoni "B" Wilaya ya Ilala Dar es Saalam Mikidadi Shabani (37) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya manila.

Jiji latakiwa kujenga miundombinu

Na Benedict Kaguo,Tanga


MBUNGE wa zamani wa Viti Maalum CUF Bi Nuru Awadh Bafadhili ameutaka uongozi wa jiji la Tanga kujenga miundombini ya maji taka ili kuwawezesha wananchi kupata mahali pa kumwagia maji taka tofauti na ilivyo sasa.

'Wakulima epukeni ugonjwa wa batobato


Na Livinus Feruzi
Bukoba.

WAKULIMA wa zao la mhogo katika maeneo ambayo tayari yameathirika na ugonjwa wa Batobato kali, wametakiwa kuepuka matumizi ya mashina ya mihogo yaliyokomaa wakati wa upandaji wa zao hilo ili kuepuka kuendelea kuenea kwa ugonjwa huo.

MSAADA




Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Barclays Tanzania, Daniel Mbotto (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 2.4 na vyakula mbalimbali kwa Mkuu wa Kituo cha Don Bosco cha Kimara, Evans Tegete, Dar es Salaam jana, vilivyotolewa na benki hiyo kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo hicho. Fedha hizo zitalipia karo za shule kwa watoto hao. (Na Mpigapicha Wetu)

NDC kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe



Na Agnes Mwaijega

SHIRIKA la Maendeleo la Taifa (NDC) limesema limejipanga kuhakikisha linazalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe ili kupunguzu tatizo la nishati hiyo nchini.

Wawili wafariki dunia Dar



Leah Daudi na Angelina Faustine

WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti Jijini Dar es salaam, likiwemo la mtoto Praygod Emanueli(1) kudumbukia kwenye shimo la maji na kufariki papo hapo.

MJI MPYA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu (kushoto) akimsikiliza Mtafiti wa Mambo ya Asili na Utamaduni kutoka Ufaransa, Nicholas Hubert (wa pili kushoto), wakati wa maonesho ya vivutio mbalimbali vya Mji Mpya wa Kilwa, mkoani Pwani, yaliyofanyika kwenye Kituo cha Utamaduni wa Ufaransa, Alliance De Francaise, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Maofisa wa Halmashauri ya mji huo. (Picha na Charles Lucas)

21 November 2012

KESI YA MAUAJI DAR Wanajeshi 3 kunyongwa *Ni wale waliomuua mtoto wa Chifu Fundikira *Watiwa hatiani kwa ushahidi wa kimazingira


Na Rehema Mohamed

HUZUNI na vilio jana vilitawala katika Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam, baada ya mahakama hiyo kutoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa washtakiwa watatu waliotiwa hatiani
katika kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira ambaye ni mtoto
wa marehemu Chifu Abdallah Fundikira.

SAKATA MFUNGWA WA SMG Polisi kuanika kila kitu leo


Na Suleiman Abeid, Shinyanga

JESHI la Polisi mkoani Simiyu, limekanusha madai ya Jeshi la Magereza kuwa mfungwa aliyehukumiwa miaka 15 mwaka 2010, Bw. Masanja Maguzu (42), alikamatwa uraiani akiwa silaha za kivita baada ya kumaliza kifungo chake gerezani.

Zitto alipuka tena sakata la ufichaji fedha Uswisi



Na Angelina Faustine

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Kabwe Zitto, amepingana na kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bw. George Mkuchika kuwa, Serikali ya Uswisi imeitaka Tanzania kupeleka majina ya watu wanaotuhumiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini humo kama sharti la kusaidia uchunguzi wa tuhuma hizo.

Uamsho Z'bar washauriwa kufungua kesi




Na Mohammed Mhina, Jeshi la Polisi Zanzibar

MAHAKAMA Kuu ya Vuga mjini Zanzibar, jana imetoa ushauri kwa viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislamu visiwani humo ambao wanakabiliwa na makosa ya kuhatarisha usalama wa Taifa na kudai kama hawajatendewa haki gerezani wafungue kesi ya madai.

Jina la Katibu Mkuu Kilimo sasa latumika kutapeli watu



Na Mariam Mziwanda

WIMBI la utapeli wa kutumia majina ya wakubwa serikalini, sasa limeshika kasi na kuibukia katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika baada ya baadhi ya watumishi wa taasisi zilizopo chini
ya Wizara hiyo, kunusurika kutapelewa.

AJALI


Wakazi wa jiji wakipita kando ya gari Toyota Canter namba T 612 BHY, lililopinduka baada ya kugongana na gari jingine Toyota Canter namba T 529 AAY (halipo pichani). Ajali hiyo ilitokea eneo la Buguruni Barabara ya Mandela, Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)

Vodacom yakabidhi bil. 8/- kwa JK


Na Rose Itono

RAIS Jakaya Kikwete, jana amepokea hundi ya sh. bilioni nane kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kuikabidhi katika Hospitali ya CCBRT, ili kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya huduma za uzazi na watoto.

MCHANGO

Rais Jakaya Kikwete akionesha mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 8, zilizotolewa
na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom kwa ajili ujenzi wa jengo la wodi ya wanawake katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo bW. Rene Meza, kulia ni Mkurugenzi wa CCBRT Bw. Erwin Telemans. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha, Bi. Janeth Mbene. (Picha na Mpigapicha wetu)

Wahukumiwa miaka 15 kwa kuingia hifadhini bila kibali


Na Mwandishi Wetu, Babati

MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, Wilaya ya Babati, mkoani Manyara, imewahukumu wakulima watatu kwenda jela miaka 15
na kulipa sh. milioni mbili kila mmoja wakimaliza kifungo hicho baada ya kupatikana na hatia ya kuingia katika Hifadhi ya Taifa
ya Tarangire bila kibali.

MSIBA

Rais Jakaya Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha maomboleza nyumbani kwa marehemu Jackson Makwetta, Boko kwa Wagogo, Dar es Salaam jana, alipofika kutoa heshima za mwisho. Makwetta aliwahi kuwa Mbunge na Waziri katika Wizara mbalimbali.
Picha na Ikulu

Mauaji mtoto wa Fundikira hukumu yake kutolewa leo



Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa hukumu ya akesi ya mtoto wa marehemu Chifu Abdallah Fundikira,  inayowakabili MT 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi cha Mbweni na wenzake.

Elimu bure sera ya CCM - Nape *Wadau wampinga Lowassa, wadai inapotosha



Na Waandishi Wetu

SIKU moja baada ya Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, kuitaka Serikali ione umuhimu wa kutoa elimu ya sekondari bure, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa ufafanuzi wa kauli hiyo.

VIZIMBA


Baadhi ya wakazi wa Moshi Bar, wakipimiwa maeneo ya kujenga vibanda vya  biashara ndogondogo na mmiliki wa eneo hilo, Bw. Abdul Karim, kama walivyokutwa Dar es Salaam jana. Eneo hilo litatumika kama soko la muda. (Picha na Prona Mumwi)

Dkt. Slaa amgeukia Kikwete *Amtaka asitumie muda mwingi kushambulia upinzani


Na Queen Lema, Arusha

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, amemtaka Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete,
kutotumia muda mwingi kuvishambulia vyama pinzani.

Rufaa ya TANESCO kwa Dowans Desemba 5



Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA ya Rufaa Dar es Salaam, Desemba 5 mwaka huu inatarajiwa kuanza kusikiliza rufaa ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), dhidi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Dowans.

MTUHUMIWA


Wakazi wa jiji wakimdhibiti kijana huyu (katikati) aliyetuhumiwa kuiba betri katika gari lililopata ajali eneo la Buguruni, Barabara ya Mandela, Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)

Askari Pori la Kijereshi wadaiwa kuua mfugaji kwa kumpiga risasi


Na Raphael Okello, Busega

ASKARI wa Pori la Akiba la Kijereshi, lililopo katika Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara, wanadaiwa kuwashambulia kwa risasi wafugaji wa Kijiji cha Kijereshi, kumuua mmoja na mwingine kujeruhiwa vibaya.

Tume ya Katiba yamalizia mikutano yake


Na Darlin Said

TUME ya Mabadiliko ya Katiba, jana imeanza mikutano ya kukusanya maoni katika mikoa sita ukiwemo Dar es Salaam
ambayo itamalizika Desemba 19 mwaaka huu.

TUME


Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya ya Tanzania, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, akizungumza na waandishi wahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana, kuhusu mikutano 522 iliyofanyika katika mikoa 9, kulia ni Katibu wa tume hiyo, Asaa Rashidi. (Picha na Prona Mumwi)

CUF wamtaka JK asitishe upimaji ardhi



Na Mwajabu Kigaza, Kigoma

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Prodfesa Ibrahim Lipumba, amemuomba Rais Jakaya Kikwete kusitisha tathmini ya upimaji ardhi inayoendelea mkoani Kigoma kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya nchi kavu katika makazi ya watu.

Mradi wa LVEMP 11 mkombozi wa mazingira Ziwa Victoria


Na David Mihambi

WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, hivi karibuni alikuwa jijini Mwanza kwa ajili ya kukabidhi magari ya mradi wa Hifadhi Mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP 11)ambayo yatatumika katika kuongezea utendaji wa watumishi wa mradi huo.

UVUVI

Baadhi ya wavuvi wakiendelea na shughuli zao ufukweni mwa ziwa victoria,ni kati ya sehemu ya watu wanaonufaika kupitia mradi wa Hifadhi Mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP 11), kwa kupewa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kujiepusha uvuvi wa kutumia zana zisizoruhusiwa.(Picha na mtandao).

Mgimwa: Kuchelewa fedha za wahisani kunakwamisha miradi



David John na Jesca Kileo

WAZIRI wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, amesema miradi mbalimbali iliyopo chini ya Wizara yake, haitekelezwi kwa
wakati kutokana na fedha za wahisani kuchelewa kuwafikia.

CHADEMA kuwajengea uwezo viongozi wao kupitia mafunzo


Na Kassim Mahege

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinajipanga kutoa mafunzo ambayo yatawajengea uwezo viongozi mbalimbali wa chama hicho nchi nzima wakiwemo Wenyeviti na Makatibu kama hatua moja wapo ya muendelezo wa Operesheni ya
Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

Waathirika wa Kimbunga Mbagala walalamika kutotekelezewa ahadi


Na David John

WAKAZI wa Mbagala kwa Mangaya, Dar es salaam, ambao waliathirika na kimbuka kilichotokea mwaka 2011, wameitupia
lawama Serikali kwa kushindwa kutekeleza ahadi walizotoa
baada ya kaya 70 kubomolewa nyumba zao na nyingine
kuezuliwa paa zake kutokana na kimbunga hicho.

Wanafunzi wanapotoshwa masomo ya sayansi



Na Kassim Mahege

MASOMO ya Sayansi ni miongoni mwa taaluma ambayo imeleta maendeleo makubwa ulimwenguni na kutufikisha katika karne ya Sayansi na Teknolojia ambayo hatimaye tunajivunia Utandawazi.

MAABARA


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uyole mkoani Mbeya wakiwa kwenye maabara ya shule wakijifunza masomo ya Sayansi,hata hivyo pamoja na kuwapo kwa maabara  hiyo vifaa vilivyo havikidhi haja kama inayoonekana pichani.Picha kwa hisani ya mtandao

Mwenyekiti CCM Geita adaiwa kuwatisha wakaguzi Maliasili



Na Daud Magesa, Mwanza

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Geita, Bw. Joseph Kasheku, anadaiwa kuwatisha watumishi wa Kikosi Maalumu cha Maliasili na Misitu cha Kukusanya Maduhuli ya Serikali na kudai atawafukuzisha kazi baada ya kukamatwa na
mbao pamoja na vipande vya magogo zaidi ya tani tatu.

Mfanyabiashara aungua moto, afariki dunia Dar


Leah Daudi na Angelina Faustine

MKAZI wa Ukonga, Mazizini kwa Mkoremba, Wilaya ya Ilala,
Dar es Salaaam Denis Martini (42), ambaye ni mfanyabiashara, amefariki dunia baada ya kuungua na moto.

WACHUUZI


Baadhi ya wachuuzi wa mboga za majani na matunda wa Mkoa wa Arusha wakisubiri wateja kando ya Barabara ya Kijenge juzi. Ukosefu wa maeneo maalumu kwa biashara hiyo ni kero kwa wafanyabiashara hao. (Picha na Michael Machellah)

Padre: Jitokezeni kushiriki mikutano ya katiba Temeke



Na Andrew Ignas

WITO umetolewa kwa waumini wa Kanisa Katoliki, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, kujitokeza katika mikutano ya hadhara inayoandaliwa na Tume ya Kukusanya maoni ya Katiba Mpya.

Wanafunzi 3 wafunikwa na kifusi, wafariki dunia


Na Eliasa Ally, Iringa

WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi ya Kidamali, iliyopo Kijiji cha Kidamali, katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, wamekufa baada ya kufunikwa na kifusi cha mchanga uliokuwa jirani na shimo.

19 November 2012

KILIMO


Mkulima wa mahindi na mtama wa Kijiji cha Nkuhi, mkoani Singida, Abdallah Mumwi, akisafisha shamba lake ikiwa ni maandalizi ya kilimo, kama alivyokutwa na mpigapicha wetu hivi karibuni. (Picha na Prona Mumwi)

Mfungwa adakwa na silaha za kivita *Alihukumiwa miaka 15 gerezani mwaka 2010 *Haifahamiki alitorokaje, RPC ashikwa butwaa



Na Suleiman Abeid, Shinyanga

KATIKA hali isiyo ya kawaida, Jeshi la Polisi, mkoani Simiyu linamshikilia mfungwa ambaye bado anatumikia kifungo cha
miaka 15 gerezani, mkazi wa Kijiji cha Ng’wang’wali, Bw.
Masanja Maguzu (42), baada ya kukutwa na silaha za kivita.

CHADEMA wazua jambo Arusha



Na Pamela Mollel, Arusha

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilayani Arusha, kinakusudia kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliohusika na matumizi mabaya ya fedha za umma ambazo zilitumika kufanya uzinduzi wa jiji hilo hivi karibuni.

UWEKEZAJI


Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Peniel Lyimo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi cha pamoja kati ya serikali na mwekezaji kutoka China katika mradi wa ujenzi wa bandari mpya na uendelezaji wa eneo maalumu la kiuchumi la Bagamoyo mkoani Pwani. (Picha na Prona Mumwi)

RC aagiza mazao ya wananchi kufyekwa Veronica Modest na Timothy Itembe, Tarime



MKUU wa Mkoa wa Mara, Bw. John Tuppa, ameuagiza uongozi
wa Wilaya ya Tarime, kufyeka mazao yote yaliyomo na wananchi katika eneo ambalo linamilikiwa na Serikali ili kuondo migogoro
ya ardhi ya wakazi wa Kijiji cha Ng’ereng’ere na Kurutamba.

Lowassa: Elimu ya sekondari iwe bure



Na Mwandishi Wetu, Babati

WAZIRI Mkuu mstaafu, Bw. Edward Lowassa, amesema wakati umefika wakati wa Serikali ya Tanzania kutoa elimu ya sekondari bure ili wazazi waondokane na mzigo walionao.

TAKUKURU yawaburuta kortini wasimamizi mradi wa mfereji


Na Mashaka Mhando, Tanga

VIONGOZI waliokuwa wakisimamia Mradi wa Ujenzi wa Mfereji wa Maji ya Mvua, Mtaa wa Azimio jijini Tanga na Mhandisi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani humo, wamefikishwa katika Mahakamani ya Wilaya ya Tanga, wakikabiliwa na kesi ya kutumia vibaya madaraka yao.

BARAFU


Mwandishi Aidan Libenanga afariki



Na Mwandishi Wetu, Morogoro

MWANDISHI wa habari mwandamizi aliyewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali nchini likiwemo shirika la habari
nchini (SHIHATA), Aidan Libenanga (pichani), amefariki dunia jana, mkoani Morogoro kwa shinikizo la damu.

MWANDISHI AIDAN LIBENANGA AFARIKI


Lukuvi: Kuvamiwa Mapadre Iringa kusihusishwe na migogoro ya kidini


Na Eliasa Ally, Iringa

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bw. William Lukuvi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani, Wilaya ya Iringa Vijijini, amesema tukio la majambazi kuwavamia Mapadre wa Kanisa Katoliki jimboni humo na Paroko mmoja kupigwa risasi, halina uhusiano na migogoro ya kidini.

VURUGU


Askari kanzu (wa pili kulia) akimdhibiti kondakta wa basi linalosafiri kati ya Kariakoo na Gongolamboto (kulia). Kondakta huyo alituhumiwa kugombana na kondakta mwingine (hayupo pichani), kama walivyokutwa Shule ya Uhuru, Kariakoo Dar es Salaam jana. (Picha na Prona Mumwi)

Tukio la kutoroka mfungwa gerezani tunahitaji majibu



JESHI la Polisi nchini linafanya jitihada kubwa za kupambana na uhalifu pamoja na wahalifu ambao ni kikwazo cha maendeleo ya wananchi kutokana na nguvu wanayotumia kutaka utajiri wa
haraka wasioutolea jasho hata kusababisha vifo.

MGOMO



Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kwenda Zambia na mikoa ya Tanzania wakiwa katika foleni ya kurudishiwa fedha za nauli, baada ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), kugoma Stesheni ya Dar es Salaam jana. Wafanyakazi hao wanagoma kushinikiza mamlaka hiyo kuwalipa stahili mbalimbali ikiwamo mishahara. (Picha na Prona Mumwi)

MAPADRI WA ITALI WATISHIA KUKIMBIA.Ni baada ya kujeruhiwa na majambazi

Na Eliasa Ally, Iringa
November 17, 2012

Mapadre wa Misionari wa kutoka Nchini Italia wanaofanya kazi za kanisa mkoani Iringa
wametishia kuondoka baada ya padre mwenzao Angelo Burgio wa Italia kupigwa risasi na
kuporwa fedha katika parokia ya Lwang'a ambapo wamesema kuwa hali ilivyo kwa sasa ya
usalama kwa watumishi hao wa Kanisa ni mdogo na wametaka misaada yote
wanayoifadhilia kwa wananchi na waumini maeneo ya vijijini wataacha kuendelea
kufadhili.

Huu ni wakati wa Waafrika kuamka



Na Michael Sarungi

NIWAZI kuwa Bara la Afrika tangu karne ya 15 limepoteza mwelekeo na hivyo kuruhusu kuburuzwa katika kila mfumo unaoasisiwa na mataifa toka Ulaya na Marekani.

Tume ya utumishi wa mahakama tuhuma dhidi yenu hamjazijibu


NA Michael Sarungi.

KATIKA siku za hivi karibuni vyombo mbali mbali vya habari viliripoti kuwa Tume ya Utumishi wa Mahakama imemjia juu Mbunge wa Singida Mashariki,Bw.Tundu Lissu, kuhusu kauli yake ya kuwapo upungufu katika uteuzi wa majaji hapa nchini.

BOMOABOMOA


Diwani wa Kata ya Ukonga, Elizabeth Mbano (wa pili kulia) akisimamia ubomoaji wa vibaraza vya nyumba ili kupisha mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Mombasa hadi Moshi Bar uliozinduliwa Dar es Salaam jana. Ujenzi huo wa kiwango cha lami unatarajia kukamilika katika kipindi cha miezi 3. (Picha na Willbroad Mathias)