Mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda, Mhashamu Pascal William Kikoti, ukiteremshwa na baadhi ya Mapadri jana katika Uwanja wa Ngege, mjini Mpanda, mkoani Katavi, tayari kwa mazishi ambayo yatafanyika kesho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
31 August 2012
Bashe, Kigwangala watoleana bastola *Walikuwa wakirudisha fomu za NEC *Katibu CCM Nzega aamulia ugomvi
Na Allan Ntana, Nzega
KATIKA hali isiyo ya kawaida, wagombea wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, wanaowania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), wilayani hapa, wanadaiwa kutishiana bastola.
CCM: Tunaweza kuifuta CHADEMA *Wassira awaonya kutovuruga amani nchini
Na Raphael Okello, Bunda
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wassira, amesema Serikali ina uwezo wa kumuomba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. John Tendwa ili akifute Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kama kitaendeleza siasa za kuvuruga amani ya nchi.
Ngulume afariki dunia
Stella Aron na Heri Shaaban
MWANASIASA mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya mbalimbali nchini kwa miaka 18, Bi. Hawa Ngulume, amefariki dunia jana asubuhi jijini Dar es Salaam.
Mahakama yawaachia wanafunzi 51 UDSM
Na Grace Ndossa
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana imewaachia huru na kuwafutia mashtaka wanafunzi 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kufanya mikusanyiko na maandamano bila kibali.
Kujisaidia porini marufuku kuanzia kesho
Na Stella Aron
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imesema kuanzia kesho abiria na wamiliki wa mabasi yanayosafiri umbali mrefu ambayo yatakutwa porini wakichimba dawa (kujisaidia), watakamatwa na kuchukuliwa hatua.
Mshindi BSS kuzindua albamu Uwanja wa Fisi
Na Mwandishi Wetu
MSHINDI wa mashindano ya Bongo Star Search (BSS) 2009, Pascal Cassian anatarajia kuzindua albamu yake ya nyimbo za injili ya Yasamehe Bure keshokutwa Uwanja wa Fisi.
Dstv waongeza chanel mpya
Na Victor Mkumbo
KAMPUNI ya Multichoice, imezindua baadhi ya Chanel mpya ambazo zitaanza kuonekana hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Habari wa Dstv Tanzania Barbara Kambogi, alisema wameamua kuzindua chanel mpya ambazo zitawafanya wateja wao kuangalia burudani mbalimbali.
Redds Miss Mwanza, Mashariki kivumbi
Na Mwandishi Wetu
SAFARI ya kuwania taji la Redd’s Miss Tanzania 2012 inaendelea kushika kasi, ambapo leo kutafanyika mashindano ya kumsaka Redd’s Miss Mwanza na kesho Redd’s Miss East Zone atapatikana Morogoro.
WANYANGE
Wanyange wa Jiji la Mwanza wanao taraji kupanda jukwaani kesho Ijumaa Agosti 30, 2012 katika ukumbi wa Yatch Club jijini humo kuwania taji la REDD'S MISS MWANZA 2012 wakiwa katika pozi mbalimbali. Shindano hilo linataraji kuwakutanisha miamba wawili wa Miondoko ya pwani, Bibie Hadija Omar Kopa na mkongwe Mwanahawa Alli na mkali mwingine Bob Haisa.
Mwanemti kutupa karata leo PARALIMPIKI
Na Amina Athumani
MWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Walemavu ya Olimpiki (PARALIMPIKI) iliyoanza juzi jijini London, Uingereza Zaharani Mwanemti, leo anaanza kutupa karata yake ya kwanza.
Gadna G Habash sasa kurindima Times FM
Na Mwandishi Wetu
KITUO cha Redio Times FM, kinachokuja kwa kasi nchini jana kimemtangaza rasmi mtangazaji maarufu nchini, Gadna G. Habash kujiunga nao baada ya kukaa nje ya ulingo kwa muda mrefu.
UTAMBULISHO
Gadna G Habash akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Dar es Salaam jana. Wengine kushoto kwake ni watangazaji wenzake Scholastica Mazula, Clifford Ndimbo na Khadija Shaibu 'Dida'. Kulia ni Jabir Saleh. Picha kwa hisani ya bongostaz
CHANETA yafanikiwa kwa mara ya kwanza
Na Amina Athumani
CHAMA cha Netiboli Tanzania (CHANETA), kimesema kwa mara ya kwanza michuano ya Ligi Daraja la Kwanza imefanikiwa kukusanya timu nyingi zaidi, tangu kuanzishwa kwa chama hicho ikiwa ni pamoja na timu zote kulipa ada ya ushiriki.
Twite akata mzizi wa fitna *Atua Dar, atamba kufanya makubwa
Na Charles Lucas
HATIMAYE ile filamu ya beki mpya wa Yanga, Mbuyu Twite imemalizika jana baada ya kuwasili Dar es Salaam na kukata mzizi wa fitna.
NIMEKUJA
Beki mpya wa Yanga, Mbuyu Twite akiwasalimia mashabiki wa timu hiyo waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana. Katikati ni Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Selestine Mwesiga kushoto kwake ni mwanachama wa Yanga, Ahmed Seif 'Seif Magari'. (Picha na Charles Lucas)
Milovan: Sasa mina timu ya mashindano
Na Elizabeth Mayemba
KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amesema kwa sasa kikosi chake kipo tayari kucheza mechi yao ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, kwa kuwa wachezaji wake wamezoeana na wanaelewana vizuri uwanjani.
30 August 2012
Kadinda kufanya vitu vyake New York
Na Mwandishi Wetu
MBUNIFU wa Tanzania, Martin Survivor Kadinda ‘Martin Single Button’ anatarajia kuonesha mavazi yake kesho nchini Marekani katika onesho la mavazi la New York Africa Fashion Week na Music on The Caltwalk (MOC).
Mtanzania atakiwa kucheza Ujerumani
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB), kimetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Robert Makanja, ili aweze kucheza nchini humo.
BURUDANI
Washiriki wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012, Wilaya za Ilala na Kinondoni wakiwa na mmoja wa wadhamini wao 'Secrets Lingerie', wakiwa kwenye ufukwe wa Msasani. Washiriki hao kwa pamoja wanajiandaa na mashindano ya kuwatafuta wanyange watakaokwenda kushiriki fainali za Taifa. Picha na blogu ya issamichuzi
Kutambulisha mwanamuziki mpya kesho
Na Mwandishi Wetu
BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa "Wana Kibega', kesho wanatarajia kufanya onesho maalumu kwa ajili ya kumtambulisha mwanamuziki mpya ambaye hata hivyo uongozi wa bendi hiyo haujaweka wazi bedndi atakayotokea.
Wawili 'wavuta mkwanja' Mwanza
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Coca-Cola ya Nyanza Bottlers, imewazawadia washindi wa promosheni ya 'Vuta Mkwanja' zawadi ya fedha taslimu.
Serengeti Boys kuivaa Misri
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), itaivaa Misri kwenye raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 10 za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Kocha Yanga kuwekwa kiti moto
Na Zahoro Mlanzi
SIKU moja baada ya Kocha Mkuu wa timu ya Yanga, Tom Saintfeit kudaiwa kusema hajatimiziwa baadhi ya vitu katika mkataba wake na kutishia kuondoka, uongozi wa Yanga umekuja juu na kusema utamchunguza kocha huyo kutokakana na kauli alizozitoa kama ni za kweli na kisha kuangalia vitu gani ambavyo hawajamtimizia.
29 August 2012
JK aomboleza vifo vya askari watatu JWTZ
Na Mwandishi Wetu
AMIRI Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, kuomboleza vifo vya askari watatu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliokuwa wanalinda amani Darfur, nchini Sudan, ambavyo vimetokea mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mfadhili CHADEMA ahamia CCM
Na Faida Muyomba, Sengerema
MLEZI na Mfadhili Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo la Sengerema, mkoani Mwanza, Bw. Alex Manji, ametangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Polisi waua majambazi 4 Tabora
Na Frank Geofray, Jeshi la Polisi Tabora
JESHI la Polisi mkoani Tabora, limewaua majambazi wanne katika mapambano ya kurushiana risasi kati yao na polisi baada ya jaribio lao la kutaka kuvamia Congres Centre, kuzuiwa na jeshi hilo.
Washtakiwa wamkataa Hakimu
Na Rehema Mohamed
WASHTAKIWA wa kesi ya unyang'anyi wa kutumiwa siraha, jana wamemkataa Hakimu Waliyarwande Lema, anayesikiliza kesi hiyo kwa madai ya kutokuwa na imani naye.
Madaktari 50 kutoka India kutoa tiba Dar
Na Salim Nyomolelo
JOPO la madaktari 50 kutoka nchini India, wanatarajia kufanya maonesho ya matibabu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Agosti 30 hadi 31, mwaka huu, kuanzia saa nne asubuhi hadi 11 jioni.
Kagasheki asikitishwa idadi ndogo ya watalii nchini
Na Mariam Mziwanda
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amesema idadi ndogo ya watalii wanaotembelea vivutio vingi vilivyopo nchini hairidhishi hivyo kuitaka sekta binafsi kuwa mhimili wa utalii nchini.
Mrema azidi kumshtaki Kimaro
Na Gift Mongi, Moshi
MBUNGE wa Vunjo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Bw. Augustine Mrema, ameendelea kumshtaki kwa wananchi mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Bw. Aloyce Kimaro (CCM), kwa madai ya kupora ardhi zaidi ya ekari 10, zilizopo katika Mji Mdogo wa Himo wakati wa uongozi wake.
Jengo la Utawala Mombo laungua
Na Yusuph Mussa, Korogwe
JENGO la Utawala la Mamlaka ya Mji Mdogo Mombo, Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, juzi usiku limeteketea kwa moto pamoja na nyaraka zote za Idara ya Fedha, Masjala, Ofisi ya Mtendaji wa Mamlaka hiyo na Mwenyekiti wake.
Mwakyembe ataka uundwaji tume kuboresha usafiri wa reli
Na Stella Aron
TANZANIA inakabiliwa na hali mbaya ya usafiri wa reli hivyo Serikali inapaswa kuunda kamati ambayo itatoa mapendekezo yatakayoboresha usafiri huo nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Marekebisho ya Sera ya Usafirishaji nchini, Mhandisi Malima Bundala, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, kufungua warsha ya siku mbili kwa kamati hiyo.
Elimu ya kujitambua itakomesha tatizo la mimba kwa wanafunzi
TATIZO la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini, linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu.
Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinathibitisha kuwa tatizo hili limekuwa likiongezeka siku hadi siku hasa baada ya kuanzishwa shule za kata.
Ushuru utumike kuboresha miundombinu sokoni
Na Lulu Malenda
MIUNDOMBINU ni sekta muhimu inayotakiwa kupewa kipaumbele ili kuongeza kasi ya maendeleo.
Nchi zilizoendelea zimewekeza katika miundombinu ambayo ndio kitovu cha sekta zote kwani kila kitu hutegemea usafiri ili kufika sehemu husika.
Malinzi kuzindua Rock City Marathon
Na Mwandishi wetu
MICHUANO ya mbio za Rock City Marathon 2012, inatarajia kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Mbio hizo zitanduliwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Taifa Deoniz Malinzi na baadae washiriki watapata fursa ya kujaza fomu za maombi ya kushiriki.
Ghana, Niger mabingwa Rising Stars
NAIROBI, Kenya
FAINALI za michuano ya Airtel Rising Stars Afrika, zimefikia mwisho huku timu ya wavulana ya Niger na wasichana kutoka Ghana, zikinyakua ubigwa.
Michuano ya Tusker 'kutumbua' dola 450,000
Na Zahoro Mlanzi
KAMPUNI ya Bia Afrika Mashariki (EABL), imedhamini mashindano ya Kombe la Tusker kwa dola 450,000 yatakayofanyika nchini Uganda kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 8.
MAPOKEZI
Mmoja wa mashabiki wa Yanga waliofika kuilaki timu hiyo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam juzi, wakati ikitokea Rwanda kwa ziara ya kimichezo kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame akipokea Kombe la Kagame mara baada ya kuwasili. (Picha na Situ Athuman)
Uongozi Yanga wamruka Saintfeit *Ujio wa Twite giza totoro
Na Zahoro Mlanzi
SIKU moja baada ya Kocha Mkuu wa timu ya Yanga, Tom Saintfeit kutangaza kuwepo na mechi mbili za kirafiki, timu hiyo imemruka kimanga kocha huyo kwa kusema mechi wanayoitambua ni dhidi ya Coastal Union itakayocheza Jumamosi kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam.
Filamu ya Yondan, Redondo kumalizika Jumapili
Na Zahoro Mlanzi
SAKATA la wachezaji Kelvin Yondan wa Yanga na Ramadhan Chombo 'Redondo' wa Simba, linatarajiwa kufikia tamati Jumapili baada ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa kukutana kupitia usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2012/2013.
28 August 2012
CCM: Hatuiombi radhi CHADEMA *Nape asisitiza ushahidi wa kutosha upo *Wajipanga kumfikisha Dkt. Slaa kortini
Na Salim Nyomolelo
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwenda mahakamani haraka badala ya kusubiri kuombwa radhi ili kusafishwa dhidi ya madai ya chama hicho kupewa fedha na mataifa tajiri.
KERO YA MAJI
Mkazi wa Kijiji cha Matilinya, Kata ya Kwadelo, Jimbo la Kondoa Kaskazini, Bi. Esther Khamis, akichota maji kwenye dimbwi ambalo pia ng'ombe wanakunywa maji kama alivyokutwa mwishoni mwa wiki, tatizo la maji kwenye eneo hilo linatokana na uchakavu wa miundombinu iliyojengwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alipofanya ziara mwaka 1973. (Picha na Charles Lucas)
Mwanafunzi mbaroni kwa kupinga sensa
Na Anneth Kagenda
JESHI la Polisi nchini linamshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Bw. Yusuf Ernest, mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam kwa tuhuma za kusambaza ujumbe kwenye simu za mkononi ili kuhamasisha wananchi wasijitokeze kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza Agosti 26 mwaka huu.
Sera za kibenki zinazotungwa zitekelezwe kwa vitendo
Na Cornel Antony
UMASKINI uliokithiri na hali ngumu ya maisha nchini umesababisha wananchi wengi kuwa waoga na kukosa ubunifu ili kujikwamua na hali hiyo.
Pia, wengine huogopa kukopa fedha katika taasisi za fedha ili kuanzisha miradi kwa kukosa ufahamu wa mikopo.
Zao la pareto likiangaliwa upya litakuwa mkombozi kwa wakulima
Na Alfred Mwahalende
LICHA ya kilimo kuwa ni uti wa mgongo kwa watanzania wengi
bado kuna kusuasua kwa sera na utekelezaji wa mipango na mikakati inayohusu sekta hiyo.
Jitihada zinahitajika kuukomboa ushirika Mtwara
Na Cornel Antony
SHERIA ya ushirika ni mwongozo uliopo kisheria ambao umepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupewa kibali kwa kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Askari wanyamapori wadaiwa kupora fedha zaidi ya mil. 4/-
Na Said Njuki, aliyekuwa Kondoa
WAFANYABIASHARA watatu wakazi wa Kijiji cha Itolwa, Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, wameiomba Serikali kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria askari sita wa Pori la Akiba Mkungunero, kwa madai ya kuwateka, kuwatesa pamoja na kuwapora zaidi ya sh. milioni nne.
DC apoteza msafara wa Mwenge
Na Salma Mrisho, Geita
KATIKA hali isiyo ya kawaida, mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Geita, juzi ziliingia dosari baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Manzie Mangochie, kuupoteza msafara wake.
Hali hiyo ilikwamisha ukaguzi wa miradi iliyokuwa ikaguliwe na Kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Kapteni Honest Mwanossa.
SUMATRA kukusanya maoni ya wadau kuhusu kanuni za usafirishaji
Na Grace Ndossa
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), leo itakutana na wadau wa sekta ya usafirishaji abiria kwa njia ya barabara, na wananchi ili kukusanya maoni yao kuhusu mapitio ya kanuni za ufundi, usalama na viwango vya ubora wa huduma kwa magari ya abiria.
'Mamlaka ziingilie kati ubora wa mafuta'
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA zinazohusika kusimamia ubora wa mafuta ya petroli, zimetakiwa kuingilia kati na kutoa majibu sahihi ili kuondoa mkanganyiko ulioibuliwa na Shirika la Viwango nchini (TBS).
Mkanganyiko huo unatokana na TBS kutangaza kuwa, mafuta yanayotumika nchini yanaruhusiwa kuchanganywa na kemikali nyingine ikiwemo ethanol.
Halmashauri ziwe makini na fedha za miradi - RC
Na Agnes Mwaijega
HALMASHAURI zote jijini Dar es Salaam, zimetakiwa kuwa makini na usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo kwa kuhakikisha zinafuata sheria ya manunuzi na malipo.
ADC kupata cheti usajili wa kudumu
Na Rehema Maigala
CHAMA Kipya cha Siasa nchini, Alliance for Democratic Change (ADC), leo kinatarajia kupata cheti cha usajili wa kudumu baada ya kumaliza uhakiki wa wanachama katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Hukumu ya Mtikila yasogezwa mbele
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana imesogeza mbele hukumu ya kesi ya kuchapisha na kusambaza walaka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, hadi Septemba 6 mwaka huu.
TFDA yaandaa mafunzo wataalamu wa maabara
Na Heri Shaaban
MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), jana imezindua mafunzo ya siku tatu ya wataalamu wa maabara kutoka nchi 13 za Afrika ambayo yameandaliwa na mamlaka hiyo.
HATARI
Gari Toyota namba T 145 ARU, likipita kando ya tawi la mti lililowekwa katika chemba ya maji ikiwa ni tahadhari kutokana na kutokuwapo mfuniko, kama lilivyokutwa makutano ya Barabara za Ohio na Samora, Dar es Salaam jana, mifuniko imekuwa ikiibwa na watu wasiofahamika na kuuzwa kama chuma chakavu. (Picha na Charles Lucas)
Wanne wafariki katika matukio tofauti Dar
Neema Kalaliche na Mariam Said
WATU wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti yaliyotokea jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, alisema katika tukio la kwanza, mtoto Yaisi Mohamed (6), alikufa papo hapo baada ya kukanyagwa na gari wakati dereva wake akilirudisha nyumba bila kumuona.
'Wapuuzeni watu, vikundi vinavyotaka kukwamisha sensa'
Tumaini Maduhu na Andrew Ignas
MKUU wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, Bi. Regina Mgema, amewataka wananchi wilayani humo kuwa makini na kuwapuuza watu au vikundi vinavyoshawishi wasishiriki Sensa ya Watu na Makazi ili Serikali ishindwe kupanga mikakati ya maendeleo.
Yanga yatua nchini bila Twite *Kutua leo kuikabili Mafunzo
Na Zahoro Mlanzi
MABINGWA wa Kombe la Kagame, Yanga wametua nchini jana wakitokea Rwanda huku Kocha Mkuu wa timu hiyo, Tom Saintfeit akimsifia beki wake mpya, Mbuyu Twite kutokana na uwezo aliouonesha na ametamba atamuanzisha katika mechi ya kesho dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.
27 August 2012
Pinda awaondoa hofu wenyeviti *Makarani Ilala wagomea sensa hadi kieleweke
Na Mwandishi Wetu, Katavi
WAZIRI Mkuu, Bw.Mizengo Pinda, amesema posho za wenyeviti wa vitongoji na vijiji ambao wataambatana na makarani wa Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza jana, zipo palepale hivyo hakuna sababu ya kujenga hofu juu ya malipo yao.
Karani wa sensa auawa, aporwa fedha sh. 200,000
Na Patrick Mabula, Kahama
KARANI wa sensa ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Kawe, iliyopo Kata ya Kilago, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, Stanley Mahene, ameuawa na watu wasiofahamika na kuporwa sh.200,000, alizolipwa baada ya kuhudhuria mafunzo ya sensa.
Gharama elekezi za Sekta ya Ulinzi Binafsi
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Sekta ya Ulinzi Binafsi nchini (TSIA), kimetangaza viwango vipya vya gharama elekezi kwa shughuli za ulinzi wa kampuni binafsi zinazotumia kiwango cha mshahara sh.80,000.
DC Lushoto ahadharishwa na wananchi
Na Yusuph Mussa, Lushoto
BAADHI ya wakazi wa Kata ya Vuga, Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga, wamesema Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw.Majjid Mwanga hatafanikiwa kuzuia uharibifu wa mazingira na uvunaji haramu wa mazao ya misitu, kama wenyeviti na watendaji wa vijiji katika kata hiyo wataendelea kubaki madarakani.
KUVUNJA SHERIA BARABARANI
Mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda jijini Dar es Salaam, ambaye jina lake halikufahamika akiwa chini ya ulinzi baada kukamatwa na askari akidaiwa kuvunja sheria za usalama barabarani katika Barabara ya Uhuru, mwishoni mwa wiki. (Picha na Anna Titus).
Serikali yadaiwa kutelekeza watu 5,000
Na Said Njuki, Babati
ZAIDI ya wakazi 5,000 wa Vijiji vya Ayamango, Gedamar na Gejedabugh, Wilaya ya Babati, mkoani Manyara, wanadaiwa kutelekezwa na Serikali wakidaiwa kuishi ndani ya eneo la Hifadhi ya Taifa Tarangire, iliyopo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), kinyume cha sheria kwa zaidi ya miaka 50.
Mbinu za kuondokana na msongamano, foleni Dar
Na Mwandishi Wetu
TATIZO la msongamano wa magari katika barabara mbalimbali jijini Dar es Salaam, limekuwa likiongezeka siku hadi siku.
MIKOPO
Baadhi ya Wakulima wa Vijiji vya Kwadelo, Matilinya na Kelelechang'ombe, Kata ya Kwadelo, Jimbo la Kondoa Kaskazini, mkoani Dodoma, wakiangalia baadhi kati ya matrekta 64 aina ya Farmtrac kwenye viwanja vya hadhara juzi, waliyokopeshwa ili kutekeleza mpango wa Kilimo Kwanza kwenye kata hiyo. (Picha na Charles Lucas)
Waliomliza DC Nkasi kamwe wasichekewe, wachukuliwe hatua
MWISHONI mwa wiki, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, Bw. Idd Kimanta, aliangua kilio kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani mjini Namanyere, baada ya kusikitishwa na utendaji mbovu wa Mkurugenzi pamoja na Wakuu wa Idara mbalimbali.
Serikali kuwafikishia huduma za simu wananchi-Dkt.Mgimwa
Na Eliasa Ally, Iringa
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Dkt.William Mgimwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kalenga mkoani Iringa amesema Serikali itahakikisha wananchi ambao hawafikiwi na mawasiliano ya simu za mkononi hususan katika maeneo ya vijijini inawajengea minara.
Mtoto anusurika kuibwa
Na Mwandishi Wetu, Bukoba
MTOTO wa miaka miwili na nusu, Vanesa Victor, amenusurika kuibwa na watu wasiojulikana waliofika nyumbani kwao wakiwa ndani ya teksi na kumtaka apande ili wampatie soda.
BURUDANI
Wasanii wa Kikundi cha Kwaya cha The Tanzanite Eagles cha Benki ya Barclays, wakifanya onesho maalumu kwenye ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Urusi, Dar es Salaam juzi, wakijiandaa kwa safari ya Afrika Kusini, ambako watashiriki onesho la kwaya kwa vikundi vya nchi za Afrika. (Na Mpigapicha Wetu)
DAAA yatamba kung'ara mashindano ya Taifa
Na Amina Athumani
CHAMA cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAAA), kimetamba kufuta uteja katika mashindano ya Taifa ya mchezo huo na kwamba watahakikisha wanavunja rekodi kwa mkoa huo.
Miss East Afrika sasa kufanyika Des. 7
Na Neema Kalaliche
MASHINDANO ya Miss East Afrika kwa mwaka huu, yamepangwa kufanyika Desemba 7 badala ya Septemba katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam na yanatarajiwa kurushwa 'live' kupitia M-Net.
Nyota wa kikapu NBA akoshwa na vipaji nchini
Na Amina Athumani
NYOTA wa timu ya mpira wa kikapu ya Chicago Bulls inayocheza Ligi Kuu ya mchezo huo Marekani (NBA), Luo Deng ameridhishwa na uwezo wa chipukizi wa Tanzania baada ya kuwaona katika kliniki inayoendeshwa na Mtanzania, Hashim Thabit anayechezea ligi hiyo pia.
Simba yazuru TBL Arusha
Na Mwandishi Wetu, Arusha
TIMU ya Simba ambayo imeweka kambi mkoani Arusha, imefanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha kutengeneza Bia Tanzania (TBL) kilichopo jijini hapa.
TBL
Mratibu wa Usalama na Afya wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kassena Heavy (kushoto), akiwaeleza jambo wachezaji na viongozi wa Klabu ya Simba waliotembelea Kiwanda cha TBL kilichopo Arusha mwishoni mwa wiki, ili kujionea uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro Lager ambayo ndio mdhamini wao mkuu. (Picha na Executive Solutions)
BFT yaomba maandalizi mapema Olimpiki 2016
Na Amina Athumani
SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limeiomba Serikali kuanza maandalizi mapema ya Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 itakayofanyika nchini Brazil, ili kuepuka kujirudia kufanya vibaya kwenye michezo hiyo.
Tanzania yatoka kapa Zone 5 kikapu
Na Amina Athumani
TIMU za Tanzania zilizokuwa jijini Kampala, Uganda kwenye mashindano ya Zone 5, yanayoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu (FIBA), zimeondoshwa kwenye michuano hiyo.
Timu hizo ni ABC na Savio kwa timu za wanaume na Jeshi Stars na Don bosco kwa timu za wanawake.
MAADHIMISHO
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim, Bw. Yogesh Manek akishikwa mkono na moja wa wakurugenzi wa Bodi ya benki hiyo, Bw. Juma Mwapachu (kushoto), wakati wa sherehe ya wafanyakazi kuadhimisha, Miaka 15 tangu kuanzishwa iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, (Wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Anthony Grant. (Na Mpigapicha Wetu)
Yanga we acha tu Kigali *Yaichapa Polisi 2-1 *Simba anguruma Arusha
Na Zahoro Mlanzi
MABINGWA WA Kombe la Kagame, timu ya Yanga, imeendeleza wimbi la ushindi katika kambi iliyoweka jijini Kigali baada ya kuichapa Polisi Force ya jini humo kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa kwenye Uwanjwa Stade de Kigali.
Watoto wa kike watakiwa kujitambua
Na Victor Mkumbo
WANAWAKE wenye umri chini ya miaka 18, wametakiwa kujitambua ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Akizungumza katika Semina ya waschana wenye umri wa kuanzia miaka 11 mpaka 18 juzi, Mkurugenzi wa Shirika la TWA, Irene Kiwia alisema kuwa vijana wanatakiwa kujitambua ili kuweza kufikia malengo.
Polisi wafichua hujuma ya sensa *Wabaini uwepo wa kikundi kilichopanga kuivuruga
Stella Aron na Anneth Kagenda
JESHI la Polisi nchini limedai kubaini uwepo wa kikundi cha watu ambao wanajipanga kuvuruga Sensa ya Watu na Makazi ambayo imepangwa kuanza usiku wa kuamkia Agosti 26 mwaka huu.
Katibu CHADEMA Morogoro ajiuzulu
Na Lilian Justice, Morogoro
KATIBU wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Morogoro, Bw. Abeli Luanda, jana ametangaza kujiuzulu wadhifa huo kwa madai ya kutoridhishwa na utendaji mbobu wa chama hicho ngazi ya Mkoa na Taifa.
Dkt. Slaa amtuhumu Kikwete
Na Goodluck Hongo, Morogoro
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kusaini posho, marupurupu ya wabunge na kushindwa kuongeza mishahara ya watumishi wa kada nyingine, kinaweza kuing'oa Serikali yake madarakani.
CUF: Siasa chafu Arusha hatuzitaki
Na Said Njuki Arusha
CHAMA Cha Wananchi (CUF) mjini Arusha, kimewataka wakazi wa jiji hilo kuwa makini na siasa za kupakana matope ambazo haziwezi kuleta tija katika maisha yao.
Wavuvi waokolewa Z'bar, mmoja afariki dunia
Na Mohammed Mhina, Jeshi la Polisi Zanzibar
WAVUVI wawili raia wa nchi jirani ya Komoro, wameokolewa kwenye kisiwa kidogo cha Pungume, nje kidogo ya Zanzibar wakiwa hoi kutokana na uchovu, njaa baada ya kupotea baharini siku 11 bila kula chakula wakiwa na boti ndogo ambayo iliishiwa mafuta.
24 August 2012
Mwakyembe aibua ufisadi bandarini *Mkurugenzi Mkuu asimamishwa kazi na wengine watatu *Kisa utendaji mbovu, wizi, rushwa, uchunguzi waendelea
Na Agnes Mwaijega
WAZIRI wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), kuwasimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Bw. Ephrahim Mgawe na wasaidizi wake watatu kwa tuhuma za wizi, rushwa na utendaji mbovu.
MWEKYEMBE
Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe akitoa tamko la kuwasimamisha kazi baadhi ya Watendaji wa Mamlamka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)Dar es Salaam jana, hatua hiyo imechukuliwa kufuatia tuhuma za wizi, rushwa na utendaji mbovu. (Picha na Heri Shaaban)
Mramba akiri kutoa msamaha
Na Grace Ndossa
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Bw. Basil Mramba, amekiri kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart, iliyoletwa na Serikali ili kufanya ukaguzi wa hesabu katika migodi ya dhahabu nchini kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za mkataba.
Papaa Msofe aumwa, kesi yaahirishwa
Na Grace Ndossa
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana imeshindwa kusikiliza kesi inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini hapa, Bw. Marijani Msofe (50), maarufu 'Papa Msofe', kwa sababu mshtakiwa anaumwa.
Machinga Complex wamjibu Masaburi
Na Zourha Malisa
BODI ya Wakurugenzi Jengo la Machinga Complex, imeshtushwa na taarifa iliyotolewa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masaburi, kuwa Jiji hilo linakusudia kumuomba Rais Jakaya Kikwete, aruhusu jengo hilo lichukuliwe na Serikali.
Mishahara ya walinzi sekta binafsi yapanda
Jesca Kileo na Darlin Said
CHAMA cha Sekta ya Ulinzi Binafsi nchini (TSIA), kimetangaza viwango vipya vya mishahara ya walinzi wa kampuni binafsi ambayo imepanda kwa zaidi ya asilimia 100.
Muhongo: Tutaendelea kusafirisha mchanga wa dhahabu nje ya nchi
Na Raphael Okello, Bunda
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema Serikali itaendelea kusafirisha mchanga ya madini nje ya nchi ili ukafanyiwe uchunguzi kutokana na ukosefu wa maabara zenye uwezo wa kubaini aina mbalimbali za madini nchini.
Hakimu akwamisha kesi ya kusafirisha binadamu Yemen
Na Grace Ndossa
KESI inayohusu biashara haramu ya kusafirisha binadamu nchini Yemen inayomkabili mfanyabiashara mkazi wa Arusha, Bw. Salim Ally, imeahirishwa kwa sababu hakimu anayeisikiliza Bw. IIvin Mgeta, kupata udhuru.
Kagasheki aongeza uwazi Malisili
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amebadili taratibu za kuwapata wajumbe wa bodi mbalimbali zilozopo chini ya Wizara hiyo.
Majenerali watatu JWTZ kuagwa leo
Na Mwandishi Wetu
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), leo litawaaga Majenerali wake ambao wamestafu jeshi kwa mujibu wa sheria.
NBC kutumia fursa za kiuchumi kupiga hatua
Na Godfrey Ismaely
BENKI ya NBC, imesema licha ya changamoto zilizopo katika ushindani wa kibiashara na uwekezaji, bado kuna fursa nyingi za masoko ambapo hali hiyo inaweza kuifanya benki hiyo iweze kujiimarisha na kukua zaidi kibiashara nchini.
Umakini wa makarani wa sensa utafanikisha kazi hiyo
Na Suleiman Abeid
AGOSTI 26, 2012 ni siku muhimu nchini kwa watanzania kutokana na sensa yanye nafasi kubwa katika taifa, kwani itawezesha serikali kupanga bajeti kulingana na idadi ya watu.
Sensa imesubiriwa kwa kipindi kirefu ikiambatana na semina, mafunzo na hamasa kwa wananchi juu ya umuhimu wake kwa maendeleo ya Taifa.
Uboreshaji maduka ya dawa, kuimarisha afya za wananchi.
Na Willbroad Mathias
MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini(TFDA), kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na shirika lisilo la kiserikali la Marekani la Management Science for Health (MSH), imekuwa ikitekeleza Mpango wa Kuboresha maduka ya dawa Baridi (DLDBs) ili yawe ya dawa Muhimu (ADDO).
Mpango huu umekuwa ukitekelezwa kupitia fedha za serikali na wafadhili na hadi sasa mikoa 18 kati ya 25 nchini imefikiwa na mpango huu.
Kingoile apeta usaili Kilimanjaro
Na Elizabeth Mayemba
ALIYEWAHI kuwa kiongozi wa zamani wa Klabu ya Villa Squad, Ally Kingoile amepita katika usaili wa wagombea uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo anagombea nafasi ya Katibu Msaidizi.
Nyilawila ajichimbia Mbeya
Na Mwali Ibrahim
BONDIA Karama Nyilawila, ameamua kuhamishia kambi yake mkoani Mbeya akiwa na lengo la kujiandaa vizuri na pambano lake dhidi Francis Cheka.
UTAMBULISHO
Msanii wa muziki wa dansi nchini Kalala Junior (katikati), akicheza na baadhi ya wanenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta wakati alipotambulishwa kujiunga na bendi hiyo Dar es Salaam jana. (Picha na Victor Mkumbo)
Kalala Junior arudi Twanga Pepeta
Na Zahoro Mlanzi
MSANII nyota wa muziki wa dansi nchini, Kalala Hamza 'Kalala Junior', amerejea katika bendi yake ya zamani, African Stars 'Twanga Pepeta'.
Msanii huyo ameamua kurudi rasmi katika bendi hiyo, baada ya kuondoka kwa miaka kadhaa ambapo alijiunga na bendi ya Mapacha Watatu.
AY, Papa Wemba, 2face jukwaa moja
Na Mwandishi Wetu
WANAMUZIKI nguli Afrika, wataungana na msanii mahiri wa kizazi kipya nchini Ambwene Yessaya, kutumbuiza wakati wa mechi ya fainali ya michuano ya Airtel Rising Stars, itakayopigwa kesho Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
23 August 2012
Vunja na Vurugu
Mramba amtaja Mkapa kortini *Ni katika kesi ya kutumia madaraka vibaya *Adai ndiye aliyebariki ujio Kampuni Alex Stewart *Chenge, Cheyo, Gavana kumtetea mahakamani
Na Grace Ndossa
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Bw.Basil Mramba, anayekabiliwa na kesi ya kutumia vibaya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya sh.bilioni 11.7, ameanza utetezi wake ambapo amemtaja Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Bw.Benjamin Mkapa kuwa alibariki Kampuni ya Alex Stewart kuingia nchini.
Mchuano wa urais 2015 waibukia Hanang'
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kile kinachohusishwa na urais wa mwaka 2015, hali ya kisiasa wilayani Hanang' mkoani Manyara imezidi kuwa tete huku kauli za wanasiasa vinara wilayani humo zikiibuka siku hadi siku.
CCM ijipange Igunga-Sitta *Ofisi ya Bunge yamlilia Dkt.Kafumu, NEC yanena
Na Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kutengua matokeo ya uchaguzi ya Jimbo la Igunga, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Jimbo la Urambo mkoani Tabora kwa tiketi ya CCM, Bw.Samuel Sitta, amewataka wana-CCM kuheshimu uamuzi huo na kuendelea kujipanga.
DC Serengeti afariki, Rais Kikwete amlilia
Na Veronica Modest, Musoma.
MKUU wa Wilaya ya Serengeti, Bw.James Lyamungu, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kutokana na kifo hicho, Rais Jakaya Kikwete, amemtumia Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw.John Tupa, salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Bw.Yamungu kilichotokea alfajiri ya jana MNH.
Subscribe to:
Posts (Atom)