27 January 2012

WAKAZI WA DAR WALIA NA MFUMUKO WA BEI.

Na Rachel Balama

WANANCHI wa maeneo mbalimbali Jijiji Dar es Salaam wamesikitishwa na mfumuko wa bei za bidhaa muhimu kwani hali  hiyo inawaweka katika wakati mgumu

SERIKALI IUNDE CHOMBO CHA KUDHIBITI BEI -GDSS

Na Rose Itono

WADAU wa semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) wameitaka serikali kuwa na chombo maalumu cha kudhibiti bei za bidhaa ili kuwawezesha wananchi wa kumudu gharama za maisha.

SERIKALI, MADAKTARI WAFIKISHANA PABAYA.

Serikali, madaktari wafikishana pabaya


*Sasa wapashana kupitia vyombo vya habari pekee
*Wagonjwa wataabika, ndugu wahaha kuwahamisha
*Watangaza athari za mgomo ndani ya siku 12

CHEKA,NYILAWILA KUPIMA UZITO LEO.

Na Mwali Ibrahim

MABONDIA Karama Nyilawila na Francis Cheka leo wanatarajia kupima uzito kwa ajili ya kujiandaa na pambano lao lisilo kuwa la ubingwa linalotarajia kufanyika kesho.

26 January 2012

MAHAKAMA KUU KUANZA KUSIKILIZA KESI YA ALIYEKUA MGOMBEA URAIS WA BURUNDI.

Na Grace Ndossa

MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam  itaanza kusikiliza kesi ya kumshikilia  aliyekuwa mgombea urais nchini Burundi Bw. Alex Sinduhije Febuari 6 mwaka huu.

MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM KUTOA MAAMUZI JUU YA PINGAMIZI LA DOWANS.

Na Grace Ndossa

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesema itatoa uamuzi wa pingamizi lililowasilishwa na Kampuni ya  Dowans la kuitaka mahakama hiyo isiwape Tanesco kibali cha kukataa rufaa Febuari 16 mwaka huu .

KATIBU MKUU TUCTA AWATAKA MADAKTARI KUTOKURUDI NYUMA KWA MADAI YAO.


Na Rehema Maigala

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Nicholaus Mgaya  amewataka madaktari wasirudi nyuma katika maslahi ya kuomba haki yao mpaka pale kitakapoeleweka.

BENKI YA KCB YATOA MISAADA KWA HOSPITALI YA BUGURUNI NA CCBRT.

Na Rehema Mohamed

BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa mbalimbali vya hospitali katika hospitali ya Buguruni na CCBRT vyenye zaidi ya thamani ya sh.milioni 22.3

SERIKALI imeshauliwa kutimiza malengo ya Milenia

Na Rehema Mohamed

SERIKALI imeshauliwa kutimiza malengo ya Milenia na mpango wa sera ya afya ili kupunguza vivyo vya watoto ambavyo vinavyoweza kuzuilika.

AZAM FC YAINYWESHA AFRICAN LYON 2-1

Na Speciroza Joseph

TIMU ya Azam FC, jana ilitoka kifua mbele katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuichapa African Lyon, mabao 2-1 iliyopigwa Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Dar es Salaam.

25 January 2012

'Wafanyabiashara Mbeya acheni kuibia serikali'

Na Esther Macha, Mbeya

WAFANYABIASHARA  wa Mbeya wameshauriwa  kuacha kuibia serikali mapato baada ya kupangishwa na halmshauri na wao kupangisha watu wengine bila kulipa ushuru .

Uchumi kwa waathirika wa vipodozi kushuka

                           
Na Esther Macha,
Mbeya

MKURUGENZI Mkuu Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA )Kanda ya Nyanda za Juu  Kusini na Bw.Paul Sonda amesema  mbali na  athari za matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kuna hatari ya uchumi kushuka kwa waathirika kutokana na gharama kubwa za matibabu
na wengine kupoteza maisha.

Vijana 1600 kupata ajira Namtumbo

Na Muhidini Amri
Ruvuma

KAMPUNI inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya Uran ya Mantra Tanzania Ltd iliyopo Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma  imesema itatoa ajira kwa vijana 1600 kutoka vijiji mbalimbali baada ya kupatiwa kibali cha kuanza kazi ya uchimbaji.

Kampuni zashauriwa kujiunga na 'Bacordes'

Na  Agnes Mwaijega

KAMPUNI na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini wametakiwa kujiunga na mfumo mpya wa kuweka alama za utambulisho za mistari 'Bacordes' katika bidhaa zao ili kuongeza kiwango cha manunuzi ya bidhaa hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari kuingia kwenye makazi ya watu ulivyobomoka kutokana na mawimbi makali katika Mji wa Pangani Kivukoni, wakati wa ziara yake mkoani Tanga jana,  ukuta huo ulijengwa miaka 100 iliyopita, kubomoka kwa ukuta huo kunatishia usalama wa wakazi wa eneo hilo. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Na Rachel Balama

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyarandu amesema kuwa nchi haiongozwi kwa wizi, ufisadi bali inaongozwa kwa kufanyakazi kwa bidii na ataendelea kuchapa kazi si kwa kutafuta urais bali kwa kujitolea ili kumsaidia rais na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.

CAF yairudishia TFF mzigo wa Simba, Yanga

Na Zahoro Mlanzi

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limesema halina matatizo na mechi za marudiano za kimataifa za Simba na Yanga, kusogea mbele ila Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lizungumze na vyama vya soka vya nchi husika.

MOTO wateketeza Nyumba na Baa katika maeneo tofauti jijini

Zourha Malisa

MOTO wateketeza Nyumba na Baa katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam ikiwemo Bw. Anna Lusiba (52),mkazi wa Mikocheni B,  moto kuzuka ghafla.
Wasukuma mikokoteni wakiwa wameketi juu ya mikokoteni, wakati wakisubiri mizigo kando ya Barabara ya Mosque, Dar es Salaam jana. wingi wa vyombo hivyo katikati ya jiji kunachangia msongamano barabarani. (Picha na Charles Lucas)

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam-yatoa Amri

Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa amri ya kuitaka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali na ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kufika mahakamani hapo kwa ajili ya kuieleza Mahakama hiyo uhalali wa kumkamata na kumshikilia aliyekuwa mgombea urais nchini Burundi Bw.Alex Sinuhnje (46).

Mshambuliaji wa Tunisia, Youssef Msakni (kushoto) akimtoka beki wa Morocco, Badr El Kaddouri wakati wa mechi za Kundi C za fainali za Mataifa ya Afrika, iliyofanyika juzi Uwanja wa Stade De L'Amitie,Libreville, Gabon.Tunisia ilishinda mabao 2-1.(Picha na AP).

24 January 2012

Dkt. Bilal
Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ilulu, mkoani Lindi, baada ya kuzindua rasmi, Bwalo la shule hiyo, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo ya Mkoa huo juzi. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)

Equatorial Guinea waitia nguvu Gabon

LIBREVILLE, Gabon

USHINDI ilioupata Equatorial Guinea dhidi ya Libya umewatia matumaini wenyeji wenzao Gabon katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012.

Kocha Sudan adai wasiwasi uliwaponza

LIBREVILLE, Gabon

KOCHA wa Sudan, Mohamed Abdalla ametaja sababu kubwa iliyochangia timu yake kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ivory Coast ni kucheza kwa wasiwasi dhidi ya wapinzani wao.

Kocha Libya asikitika kupoteza mechi

MALABO, Equatorial Guinea

KOCHA wa Libya, Marcos Paqueta amesema itakuwa vigumu  kutosikitika baada ya kupoteza mechi kwa kufungwa bao 1-0  dhidi ya Equatorial Guinea katika Kombe la Mataifa ya Afrika, Jumamosi.

Kocha Zambia ajiamini kuifunga Senegal

MALABO, Equatorial Guinea

KOCHA wa Zambia, Herve Renard ameanza kujiamini baada ya kuona timu yake ya Zambia ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senegal katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumamosi.

Mshambuliaji Burkina Faso ahangaika kujiweka sawa

LIBREVILLE, Gabon

KOCHA wa Burkina Faso, Paulo Duarte amesema kuwa mshambuliaji, Alain Traore anahangaika kujiweka fiti kwa ajili ya michuno ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 iliyoanza Jumamosi.
Kocha Polisi afurahia ushindi

Na Speciroza Joseph

KOCHA wa Polisi Dodoma, Rashid Chama amefurahia matokeo ya ushindi katika mechi yake, dhidi ya JKT Ruvu na kupanga kuendeleza ushindi ili kuiweka timu hiyo katika nafasi nzuri.

Doreen kushiriki mkutano wa uchumi duniani

Mwandishi wetu

NYOTA imeanza kung’ara kwa mbunifu wa mavazi anayekuja juu kwa kasi nchini, Doreen Estazia na lebo yake ya Estado Bird baada ya kualikwa kuhudhuria mkutano wa kujadili masuala ya Uchumi duniani (World Economic Forum) utakaonza kesho mjini Devos –Klosters, Uswisi.

Mchakato uchaguzi CHANETA kuanza Oktoba

Na Amina Athumani

MCHAKATO wa Mchaguzi Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), unatarajia kuanza Oktoba mwaka huu.

TFF yaomba makato U/Taifa yapungue

*Twiga Stars kukipiga Wabunge

Na Zahoro Mlanzi

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeiandikia barua serikali kuomba ipunguze gharama za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ya marudiano kati ya timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars) na Namibia, itakayochezwa Januari 29, mwaka huu.

Yanga yaipa ahuweni Azam FC

Na Speciroza Joseph

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema sare waliyoipata Yanga ya maboa 2-2 dhidi ya Moro United, imempa matumaini ya kukaa nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa uwiano wa pointi unazidi kupungua.

TFF yaomba makato U/Taifa yapungue

*Twiga Stars kukipiga Wabunge

Na Zahoro Mlanzi

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeiandikia barua serikali kuomba ipunguze gharama za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ya marudiano kati ya timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars) na Namibia, itakayochezwa Januari 29, mwaka huu.

Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wakicheza ngoma kwa mtindo wa Makhilkhil, inayochezwa na watu wa kabila la Waswana, Dar es Salaam juzi. (Picha na Nyakasagani Masenza) 

Migogoro ya ardhi inaweza kuepukika

Na Rachel Balama

ARDHI ni rasilimali ya msingi katika uhai wa maendeleo ya binadamu, wanyama, mimea na viumbe vyote. Nchi ya Tanzania ambayo uchumi wake unategemea kilimo kama sekta muhimu kukidhi mahitaji ya wananchi walio wengi.

Misaada kukatwa nchi zinazoendelea

*Tanzania ni ya 3 duniani kwa kupokea misaada

NCHI zinazoendelea duniani, zimetakiwa kujipanga kutokana na mdororo wa uchumi ambao umeanzia nchini Ugiriki na kusambaa katika nchi za Ulaya.

Makala-ukatili uliofanywa na mfanyabiashara mmoja maarufu mjini Arusha

Na Kassian Nyandindi, Nionavyo.


HIVI karibuni vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti juu ya
ukatili uliofanywa na mfanyabiashara mmoja maarufu mjini Arusha, juu ya
kumnyanyasa mtoto mwenye umri wa miaka 15.

WATU wawili wamefariki jijini Dar es Salaam

Na Zena Mohamed

WATU wawili wamefariki jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti likiwemo la mfanya biashara Bw. Aloyce Asenga (27),kunywa sumu.

Wafanyabiashara wadaiwa kutumia leseni za wenzao

Na Theonestina Juma,
Bukoba

WAFANYABIASHARA wasio na leseni ya biashara ya kahawa wanadaiwa kufanya biashara ya zao hilo mkoani hapa kwa kupitia mgongo wa leseni za wafanyabiashara wa kahawa wenye kibali hicho.

Madini ya shabaghafi, jasi yagundulika Singida

Na Thomas Kiani
Singida

WIZARA ya Nishati na Madini kupitia ofisi ya madini Kanda ya Kati Singida imeanza  mchakato wa kutoa elimu  kwa wananchi wa Mkoa wa Singida kuhusu rasilimali za madini ziliyoko kwenye mkoa huo baada ya kugundua kuwepo kwa madini ya shaba na Jasi wilayani Iramba na Manyoni.

NSSF yakusanya bil.16745/-

Na Queen Lema,
Arusha 

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii(NSSF)mkoani Arusha umefanikiwa kukusanya sh. bilioni 16,745 kwa kipindi cha Julay hadi Desemba 2011 ambapo fedha hizo ni sawa na asilimia 92 ya lengo walilokusudia

Ushirika washauri kushiriki katiba mpya

Na Heckton Chuwa,
Moshi

WADAU wa sekta ya ushirika nchini, wameshauriwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa katiba mpya hatua itayochangia kutoa maoni yao kuhusu masuala ya ushirika 

23 January 2012

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bw. James Mbatia, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, wakati akifafanua walichozungumza na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, kuhusu muswada wa Katiba mpya.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu (wa pili), akikagua gwaride la askari wapya 822 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wakati wa kufunga mafunzo yao ya miezi sita kwenye uwanja wa Mlale JKT jana. Kushoto ni Kamanda wa gwaride hilo Meja Aman Ramadhan.

JKT wamuomba Amiri Jeshi Mkuu kuhamasisha uwajibikaji

Na Mwandishi Maalumu, Kigoma

VIJANA wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Operesheni ya Miaka 50 ambao wamehitimu

Udhaifu wa tiba za asili wabainishwa

Na Mohamed Hamad, Arusha

WATANZANIA wameshauriwa kutumia madawa ya asili ambayo hayana kemikali yoyote

Programu masoko kusaidia wakulima vijijini

kuwafikia wananchi milioni 15


Na Ibrahimu Hamidu

SERIKALI imeazimia kuinua sekata ya kilimo nchini ili kuongeza uzalishaji
Lori la mizigo namba T 926 BUE, likishusha shehena ya mahindi kutoka mikoani, kwenye Soko la Tandale, lililoko Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam jana.

Ruvuma yapaa kilimo cha mahindi, kahawa

Na Mwandishi Wetu

SEHEMU kubwa ya maisha ya Watanzania hutegemea kilimo, kwa kutambua hivyo

Serikali yahimiza wananchi kutunza miradi ya maendeleo

Na Mwandishi Wetu, Mwanga

WANANCHI wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kulinda na kutunza

kosefu wa huduma za afya waongeza idadi ya vifo

Na Florah Temba, Moshi Vijijini

IDADI ya wagonjwa wanaofariki dunia katika Hospitali ya TPC
Mama huyu ni mfano wa kuigwa na wengine, alikutwa na kamera yetu, kando ya Barabara ya Kigogo, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam jana, akiwa amebeba beseni lililojazwa maembe, wakati akitafuta wateja pamoja na mwanae mchanga.

Uzembe wa viongozi wadaiwa kuwanyima haki wananchi

Na Zuhura Semkucha, Shinyanga

VYAMA vya siasa hapa nchini vimetupiwa lawama kwa kuwakumbatia viongozi wenye

Viti maalumu CCM watakiwa kuiga wenzao wa CHADEMA

Na Pendo Mtibuche, Dodoma

WABUNGE wa viti Maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuiga mfano

Afya ya Asamoah yazidi kuimarika

FRANCEVILLE, Gabon

MSHAMBULIAJI Asamoah Gyan  anaendelea kupona majeraha ya nyama za paja yanayomkabili

Ilala yaamisha taka zilizokaa muda mrefu

Heri Shaaban

TAKATAKA zilizokuwa zimetelekezwa katika eneo la shule ya msingi Kisukuru Kimanga
Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses (kulia) akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa Mkuu wa shule ya msingi Temeke Said Mbolembole (kushoto). Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo. Katikati ni mwenyekiti wa kamati ya shule Rajab Ndunda na Meneja wa kitengo cha mikopo benki ya Posta Abdallah Mtandika
Meneja wa kitengo cha mikopo benki ya Posta Tanzania Abdallah Mtandika akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa wadau mbalimbali kuchangia elimu ya watoto wetu kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 2 kwa shule ya Msingi Temeke.Kulia ni Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Noves Moses na mwenyekiti wa kamati ya shule Rajab Ndunda,kushoto ni mkuu wa shule hiyo Said Mbolembole.

Wanawake waandamana kupinga kuvuliwa suruali Malawi

 BLANTYRE, Malawi

WATU takriban watu 3,000 juzi walikusanyika Blantyre nchini Malawi wakiandamana kupinga

Jk,Tibaijuka watendaji hawa mnawaona?

Na Gladness Mboma

SERIKALI imekuwa ikipiga kelele kuhusu ujenzi holela hasa jijini Dar es Salaam,
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza mshambuliaji wa timu hiyo, Keneth Asamoh, baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Moro United, Uwaja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Timu hizo zilifungama mabao 2-2.
Kiungo wa Moro United, Meshack Abel, akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Kiiza, asimfikie golikipa wa timu yake, Jackson Chove, (mwenye mpira), wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Timu hizo zilifungana mabao 2-2.
Wachezaji wa timu ya soka ya Simba, wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe, Dar es Salaam jana, kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Sumari kuagwa leo Dar

Na Waandishi Wetu

MWILI wa Mbunge wa Arumeru Mashariki (CCM) Bw. Jeremiah Sumari, unatarajiwa kuagwa leo

CUF waanzisha 'changia Pemba'

Na Peter Mwenda, Pemba

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimekubaliana na wananchi waliotoka Kisiwa cha Pemba kuchanga sh. 100

CHADEMA yajibu mapigo

*Yakana kutumiwa na Ujerumani
*Dkt. Slaa asema mpaka kieleweke
*Sengerema wamvaa Ngeleja


Na Zena Mohamed

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha tuhuma dhidi yao kwamba

katizaji ruti daladala mfupa ulioshinda Polisi

Na Rose Itono

TABIA ya madereva wa daladala kukatisha ruti imekuwa ikiwasumbua wananchi kwa kuwaongezea mzigo

Zitto airarua serikali

Na Salim Nyomolelo

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC)imeishutumu serikali

Kuna tatizo la viongozi wasiowajibika

Na Peter Mwenda

SERIKALI inajitahidi kuondolea wananchi wake kero mbalimbali katika sekta

20 January 2012

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Batlda Burian, wakati Balozi huyo alipofika Ikulu Dar es Salaam jana kumuaga rasmi, baada ya kuteuliwa na Rais hivi karibubni.

Mapya yaibuka mgogoro CUF

*Wakili ataka Maalim Seif akamatwe, afungwe jela
*Awasilisha ombi la kuitwa mahakamani na wenzake

*Ni wale walioshiriki kikao cha kumtimua mteja wake
*Hamad asema CUF haina tofauti na kioo kilichopasuka


Rachel Balama na Grace Ndossa

MBUNGE wa Wawi, Zanzibar, kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Hamad Rashid Mohammed
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Sadik Mecky Sadik (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi. Susan Omar (katikati), baada ya kupokea msaada wa mabati 500 yaliyotolewa na shirika hilo, kwa ajili ya waathirika wa mafuriko, Dar es Salaam jana.

Bei mpya ya umeme sasa 'kichefuchefu'

*CTI yatoa tamko, wanaharakati waipinga, NCCR kuandamana

Agnes Mwaijega na Rose Itono

SHIRIKISHO la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), limetoa tamko la kupinga ongezeko la bei ya umeme
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Bw. Absalom Kibanda (kulia), akiwa na mwanasheria wake, Bw. Juvenalis Ngowi (katikati), nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya kesi ya kuchapisha habari za uchochezi, inayomkabilikuahirishwa jana. Kushoto ni Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Bw. Neville Meena.

Serikali, madaktari, wafikishana pabaya

Na Rehemu Maigala

MVUTANO kati ya madaktari na Serikali, sasa umechukua sura mpya na kuonekana sawa na mchezo wa kuigiza
Wakazi wa Jimbo la Wawi, Mkoani Pemba, wakimsikiliza Katibu wa vijana wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Bw. Khalifa Abdalla Ali, kabla ya kuanzisha maandamano ya kulipongeza Baraza Kuu kwa maamuzi mazito ya kuwavua uanachama, wanachama wanane, walioitwa waasi wa chama hicho hivi karibuni.

Katiba Mpya iwanufaishe wananchi katika ardhi, mazingira

Na Peter Mwenda

ASILIMIA 70 ya Watanzania wanategemea ardhi, mazingira na maliasili ili wanufaike hivyo Katiba Mpya

Tapeli aliyejifanya Katibu wa CCM ashikiliwa Polisi

Zena Mohamed na Zourha Malisa

JESHI  la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia Bw. Leonard Mwihilo

Kuna tatizo la viongozi wasiowajibika

Na Peter Mwenda

SERIKALI inajitahidi kuondolea wananchi wake kero mbalimbali katika sekta mbalimbaliikiwemo Afya, Elimu, Kilimo na Miundombinu.

Watoto wanastahili kuendekezwa kielimu

Na Rachel Balama

WATOTO ndio rasilimali yenye thamani kwa vile wao ndio wanaokabidhiwa
Mchezaji timu ya soka ya Ulongoni, Noel Nurdin(mbele), akijaribu kumtoka, juma Issa wa Gongo la Mboto FC, wakati wa mchezo wa kirafiki, uliochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ulongoni B, Dar es Salaam juzi, Ulongoni ilishinda 3-1.

Africa Lyon yaitibua TFF

Na Zahoro Mlanzi

SIKU moja baada ya timu ya African Lyon kulituhumu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Papic ataka moja kuivaa Zamaleki

Na Zahoro Mlanzi

 KOCHA Mkuu wa mabingwa soka Tanzania Bara, Kostadin Papic ameutaka uongoza wa klabu

TBL yatoa pamba Yanga, Simba SC

Na Zahoro Mlanzi

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yao ya Kilimajnaro Lager

19 January 2012

Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli, akizungumza na wakazi wa Kata ya Igunda, wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Shinyanga jana, wakati wa uchaguzi wa Chama hicho mwaka huu. Mwenyekiti wa sasa ni Bw.Hamis Mgeja
Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe kutoka Abort Fund, Bw. Andy Wilson (katikati) na Dkt. Ayub Magimba, walipomtembelea ofisini kwake, Ikulu, Dar es Salaam jana.

Madaktari kugoma

*Ni baada ya madai yao kutosikilizwa ndani ya saa 72
*Waliopo mikoani waagizwa kujiandaa na mgomo huo
 *Dkt. Nkya kuokoa 'jahazi' leo, serikali yapewa masharti

 Na Rehema Maigala

 CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT), kimewataka wanachama wake wote nchini,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Sadik Mecky Sadik (kulia), akipokea msaada vitu mbali mbali jana, vilivyotolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Posta Bw. Deos Khamisi, kwa ajili ya waathirika wa mafuriko. Wengine ni Maofisa wa shirika hilo.

Nchambi amshtaki Waziri Ngeleja Ofisi Kuu CCM

Na Rachel Balama

MBUNGE wa Kishapu, mkoani Shinyanga, Bw. Suleiman Nchambi, amemshtaki Waziri wa Nishati na Madini,

Mgomo wa malori

Waajiri wanaoghushi mikataba kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu, Tunduma

WAMILIKI wa magari makubwa ya mizigo yaendayo nje ya nchi

Maiti ya jambazi Arusha yazua 'kasheshe'

Ndugu wasusa mwili mochari, wachukuliwa na Mchungaji 

 Na Richard Konga, Arusha

NDUGU wa jambazi sugu aliyeuawa na polisi Januari 13
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Namala Mkopi, akisoma azimio la mkutano wa madaktari, Dar es Salaam jana, wakati wa mkutano huo ulijadili taarifa ya serikali, kuhusu mgogoro ulioelezwa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Lucy Nkya kwa vyombo vya habari. Kulia ni Mjumbe wa Baraza la Madaktari Dkt. Faida Emil na Makamu wa Rais chama hicho, Dkt. Primus Saidia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa Shule ya Msingi King'ongo iliyoko Kimara, ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo, Bw. Demetrius Mapesi, akizungumza na walimu wa shule hiyo, wakati wa kuwapongeza kutokana na matokeo mazuri ya mtihani wa Darasa la Saba. Kulia ni Ofisa Elimu wa Kata ya Salanga, Bi. Shahiri Hamza.

KINAPA watangaza vita kwa majangili

Na Florah Temba, Kilimanjaro

HIFADHI ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) inakabiliwa na changamoto

Gama aandaa mtego wa kuwatia hatiani wahamiaji haramu KCMC

Na Heckton Chuwa, Kilimanjaro

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw.Leonidas Gama, ameagiza uongozi wa Wilaya ya Moshi na Hospitali ya Rufaa ya KCMC,

'Soko linaharibika watendaji acheni tabia ya kukaa ofisini'

Na Theresia Victor, Dodoma

 UMOJA wa Wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba lililopo katika Manispaa ya Dodoma
Wasanii wa Nyamuswa Drama Group, Wandwi Masebe (kulia) na Aloyce Bwire, wakiigiza igizo la mzazi aliyeshindwa kuchangia gharama za shule kwa mtoto wake, wakati wa harambee ya kuchangisha fedha za madawati kwa ajili ya shule za Kata ya Nyamuswa, hivi karibuni.

Bendera mgeni rasmi pambano la Cheka

Na Mwali Ibrahim

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera anatarajia kuwa mgeni rasmi katika pambano
Baadhi ya makocha wa ngumi nchini, wakifanya mazoezi kwa vitendo wakati wa kozi ya kimataifa ya mchezo huo inayoendelea Kibaha Mkoa wa Pwani jana.

African Lyon yaipa TFF siku 30

Na Amina Athumani

KLABU ya soka ya African Lyon, imelipa siku 30 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

RT yasogeza mbele Uchaguzi Mkuu

Na Andrew Ignas

SHIRIKISHO la Riadha nchini Tanzania (RT) limesogeza mbele tarehe uchaguzi

Twiga Stars yanogewa kukaa jeshini

Na Zahoro Mlanzi

TIMU ya taifa ya wanawake (Twiga Stars), inatarajia kuingia kambini leo

Cirkovic ashusha presha Simba

Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Milovan Cirkovic anaonekana sasa kushusha presha

Madega aipa 'dawa' Yanga kuiua Zamaleki

Na Zahoro Mlanzi

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Iman Madega ameitaka timu hiyo kufanya maandalizi ya nguvu kabla haijacheza na Zamaleki

18 January 2012

Mbunge wa Vunjo mkoani Kilimanjaro kwa tiketi TLP, Bw. Augostine Mrema, akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti mkoa Morogoro, Regia Mtema, kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam jana.
Askari wa Bunge, wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti mkoa Morogoro, kwa tiketi ya Chadema, Regia Mtema, baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam jana kwa heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi (Kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Chadema, Bw. Freeman Mbowe (katikati) na Mbunge wa Ubungo Bw. John Mnyika, wakati wa kuaga mwili wa marehemu Regia Mtema, aliyeagwa kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam jana.

Mtema aagwa Dar,

wabunge 50 kuongoza mazishi yake

Na Peter Mwenda

MAKAMU wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Wwaziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, jana waliongoza mamia ya wananchi

Sakata la Posho:

Bunge lachongea
mihimili mingine

Ndugai asema watumishi wake wanalipwa zaidi ya wabunge
Awavaa viongozi wa dini, adai posho wanazolipwa ni kubwa
Azungumzia sakala la Hamad Rashid, David Kafulila, Jairo

Na Waandishi Wetu
SAKATA la nyongoza ya posho za wabunge kutoka sh. 70,000 hadi 200,000, limechukua sura mpya

Profesa Mwandosya arudi India

*Dkt. Mwakyembe aonekana ofisini mara moja
Na Gladness Mboma
WAZIRI wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, ameondoka nchini juzi kwenda India

Dawa bandia za malaria zaongeza madhara

LONDON,Uingereza

WANASAYANSI  katika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza

MECKI kuchaguana Januari 28

Na Martha Fataely, Moshi
KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro (MECKI),

Mwekezaji A to Z aomba wizara kuwapunguzia gharama

Na Mwandishi Wetu, Arusha
WIZARA ya Kazi na Ajira imeombwa kuunga mkono na kutetea viwanda vya nguo
Dkt. Nkya
Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dkt. Lucy Nkya, akizungumza na waandishi wa habari (waliosimama kulia), Dar es Salaam jana, kuhusu mgomo wa wataalamu 194 walikuwa kwenye mazoezi ya vitendo, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. (Picha na Prona Mumwi) 

Waigomea halmashauri wakitaka ipunguze ushuru

Na Esther Macha, Mbeya
Wafanyabiashara wa Soko la Soweto mkoani Mbeya jana waligoma

Ofisi ya madini mbioni kukamilika Singida

Na Thomas Kiani, Singida

WIZARA ya Nishati na Madini imekusudia kukamilisha jengo la ofisi ya madini Kanda ya Kati Singida ambalo litagharimu sh.milioni 870  hadi litakapokamilika mapema mwaka huu.

Arusha waomboleza kifo cha mdau wa maendele

Na Pamela Mollel, Arusha
OFISA Maendeleo ya Jamiii wa Manispaa ya Arusha, Bw. David Ndauka amefariki
dunia juzi jioni
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Kikapu, Alphaeus David, akiagwa na Baba yake, David Kisusi (kushoto), alipondoka Dar es Salaam jana, kwenda Nchini Canada, baada ya kupata udhamini wa kujiunga na Chuo Kikuu cha Newfounde Memorial. Kulia ni Mama yake mzazi Elizabeth Kisusi. (Picha na Nyakasagani Masenza)

Yanga kupitisha 'fagio la chuma'

Lengo ni kubana matumizi

Na Amina Athumani

UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umepanga kupunguza matumizi kwa kuwaacha baadhi ya wachezaji na kubakiza 25 pekee, badala ya 30.

Mkwassa aitolea uvivu serikali

Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars), Charles Mkwassa ameamua kuivaa serikali na kuitaka isaidie kwa kiasi kikubwa timu hiyo na si kukabidhi bendera na kuondoka.

17 January 2012

Mkuu wa kitengo cha mauzo ya Vodacom M-pesa, Bw. Franklin Bagala (kulia), akizungumza na Mawakala wa mkoa wa Dares Salaam juzi, wakati wa semina maalumu ya kuwajengea mawakala hao uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja. (Na Mpigapicha Wetu)
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam Jana kuhusu uzinduzi wa tuzo za Kill Music ambazo hufanyika kila mwaka, kulia ni Mratibu wa tuzo hizo kutoka BASATA, Luhaja Ahm. (Picha na Victor Mkumbo)

Kill Music Award yazinduliwa

Na Victor Mkumbo

KAMPUNI ya Bia Tanzania TBL, kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), jana wamezindua rasmi mchakato wa kutafuta na kuwapa tuzo wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri katika kazi zao za muziki kwa mwaka 2011.

TOC yaishangaa BFT kuishupalia Dar

Na Amina Athumani

KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC), inashangwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) kwa kushindwa kuuneza mchezo wa ngumi nchi nzima na badala yake kuishupalia Dar es Salaam pekee, wakati shirikisho hilo ni kongwe hapa nchini.

Moratti athibitisha kumtaka Tevez

ROME, Italia

RAIS wa Inter Milan, Massimi Moratti amethibitisha kuwa sasa wametuma ofa ya pauni milioni 25 kwa ajili ya mchezaji wa Manchester City, Carlos Tevez.


Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani (aliyevaa nguo nyeusi), akimbana kwa maswali
Mwenyekiti wa Kijiji cha Manga-Mtindiro Sakina Mkomwa kuhusu fedha zake alizotoa kwa
ajili ya wananchi kuvuka katika mto Mkomazi baada ya kivuko cha kuvukia wananchi
hao, kusombwa na maji kufuatia mafuriko yalitoyotokea mwishoni mwa mwaka jana kwenye
milima ya Pare wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

16 January 2012

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia), akisindikizwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Mecky Sadik kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko juzi. Kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salam Dkt. Didas Masaburi. (Na Mpigapicha Wetu)
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Samuel Sitta (kushoto) na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa (kulia), wakimfariji Bw. Estaratus Mtemanyenza, ambaye ni Baba wa Marehemu, Mbunge wa Viti Maalum, Regia Mtema, nyumbani kwao Tabata Chang'ombe, Dar es Salaam jana. (Picha na Peter Mwenda)
Rais Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma, wakitoa heshima zao za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa Kanali Pastory Kamugisha wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyefariki Dar es Salaam juzi na kusafirishwa kwenda kwao mkoani Kagera. (Na Mpigapicha Wetu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uratibu na Mahusiano na Mbunge wa Bunda, Bw. Stephen Wassira, akizungumza na umati wa wananchi wa mji wa Bunda hivi karibuni, wakati akifafanua hatua kwa hauta kuhusu mchakato wa mswaada wa katiba mpya ulivyofanyika hadi kusainiwa na Rais. Wa pili kushoto ni mbunge wa Musoma Vijijini Bw. Nimrod Mkono na Ofisa Tarafa ya Serengeti Bw. Justine Rukaka. (Picha na Nyakasagani Masenza) 

PST yamsimamisha Agapeter

Na Zahoro Mlanzi

SHIRIKISHO la Masumbwi Tanzania (PST), limemsimamisha Makamu wa Rais wa shirikisho hilo, Agapeter Mnazareth kutokana na kudaiwa kufanikisha pambano lisilo la ubingwa kati ya Karama Nyilawila na Fransic Cheka.

BMT yatakiwa kuwawezesha mabondia

Na Andrew Ignas

BONDIA wa zamani wa timu ya Taifa ya Ngumi za Ridhaa Tanzania, Michael Yomba yomba amelitaka Balaza la Michezo la Taifa (BMT), kuhakikisha linatafuta njia mbadala ya kuwawezesha mabondia wao.

Ward, Laura wasubili droo michuano Australia

Melbourne, Australia

WACHEZA tenis James Ward na Laura Robson, wamepenya hatua za awali ya michuano ya Wazi ya Australia na sasa wanasubili droo kubwa ya michuano hiyo.

Nyilawila atamba pesa mbele, mataji nyuma

Na Mwali Ibrahim

BONDIA Karama Nyilawila ameibuka na kudai kitendo cha kunyang'anywa mkanda wake wa Ubingwa wa Dunia wa WBF, na waandaaji wa mashindano hayo hakimsumbui kwani yeye anachoaangalia ni pesa.
Mafundi wakijaribu kulinasua Lori la mizigo namba T 985 AAK lililoacha njia na kugonga ukuta, kando ya Barabara ya Nyerere eneo la la Mtava, Dar es Salaam juzi. (Picha na Nyakasagani Masenza)

Botswana yatishia 'nyau' vigogo CAN 2012

GABORONE,Botswana

TIMU ya Taifa ya Botswana, imesema  itafanya maajabu makubwa kwenye fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika  kuanzia mwishoni mwa wiki hii katika nchi za Guinea ya Ikweta na Gabon, huku ikizitahadharisha timu zitakazokutana nazo kukaza buti.

Mtoto wa Wacko Jacko aanza 'mbwembwe'

LAS VEGAS, Marekani

WAHENGA walisema mtoto wa nyoka ni nyoka.

BINTI wa mwanamuziki aliyekuwa mfalme wa Pop, Michael Jackson (Wacko Jacko), Paris ameonekana kuanza kufuata nyayo za baba yake kwa kuigiza uchezaji wake ikiwemo mtindo wa kusimama kwa kutumia vidole vya mguuni wakati akicheza mpira wa magongo.

Nando atajwa kikosi cha Angola

LUANDA,Angola

MCHEZAJI Nando Rafael ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya  Angola kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika, lakini huenda hasicheze kwenye fainali hizo za mwezi huu zitakazofanyika katika nchi za Guinea ya Ikweta na  Gabon.

Ndoa ya Kobe Bryant hatarini kusambaratika

NEW York Marekani
MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant na mkewe Vanessa wako mbioni kutengana.

Ferguson akoshwa na Scholes

LONDON, Uingereza

KOCHA Alex Ferguson amempongeza mchezaji mkongwe Paul Scholes aliyemrejesha katika kikosi cha Manchester United kwa kucheza vizuri na kufunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bolton juzi.

Villa-Boas roho kwatu kwa Gary Cahil

LONDON, Uingereza

KOCHA Andre Villas-Boas amefurahishwa kwa kuwasili mlinzi Gary Cahill wakati ambao Chelsea inajianda kumtambulisha rasmi mchezaji huyo waliyemsaini kutoka Bolton.

Kocha Zambia atamba kuwa na kikosi kizuri

LUSAKA,Zambia

KOCHA wa timu ya Taifa ya Zambia, Herve Renard, amesema kuwa uwezo wa kikosi chake hauwezi kupimwa kwa matokeo ya sare ya bao  1-1 dhidi ya Afrika Kusini katika mtanange uliofanyika Jumatano mjini Johannesburg.

Zambia yatabiliwa makubwa CAN 2012

JOHANNESBURG,A.Kusini

MCHAMBUZI wa masuala ya soka katika televisheni ya  Super Sport, Thomas Kenaite, amesema kuwa timu ya Taifa za Zambia ina nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika (CAN) 2012.

'Mbaya' wa DMX akana kumshambulia

NEW YORK Marekani

MTU ambaye alidaiwa kuwa alijaribu kumshambulia rapa DMX  alipokuwa jukwaani wiki iliyopita, ameamua kusafisha jina lake kwa kusema kuwa hakutaka kumshambulia mwanamuziki huyo.

Mtu huyo aliuambia mtandao wa TMZ kwamba alichotaka kufanya usoni ni kutaka kumkumbatia kutokana na kukunwa na muziki wake.

Jamaa huyo aliyetambulika kwa jina la Andy Roy alipanda jukwaani wakari rapa DMX alipokuwa akitumbuiza Alhamisi katika eneo la Long Beach, alisema alikuwa akitaka kumpongeza nyota huyo kwa kumkumbatia.

Roy ambaye ametoka jela, alitaka kumkumbatia kuonesha kuwa wako pamoja ambapo DMX naye alitoka jela siku za karibuni.

Kwa mujibu wa Andy, ilikuwa hakuaelewaka na kuongeza kuwa, "DMX ni mgonjwa!


Mshambuliaji wa timu ya soka ya Yanga, Hamisi Kiiza (kushoto), akimtoka mlinzi wa Sofapaka ya Kenya, Abdallah Juma, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda 2-1. (Picha na Nyakasagani Masenza)
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Namala Mkopi, akisisitiza tamko la chama hicho, Dar es Salaam jana, lililoitaka Serikali kuwarudisha kazini na kuwalipa mshahara, Madaktari wanafunzi waliofukuzwa katika muda wa saa 72, kuanzia jana. Kulia ni Mjumbe wa Baraza la Madaktari Tanzania, Dkt. Faida Emil, Chama hicho pia kilimsimamisha uanachama, Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Deo Mtasiwa.

Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Maji, Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), na Mamlaka Miliki ya Miundombinu ya Maji Dar es Salaam (DAWASA), wakiangalia ujenzi wa mtambo mpya wa maji, Ruvu Chini, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Picha na Charles Lucas).

Samatta, Ochan ruksa kucheza CAF

Na Zahoro Mlanzi

HATIMAYE mshambuliaji wa timu ya taifa (Taifa Stars) na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mbwana Samatta amepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) baada ya timu yake kuomba kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Mbali na kukubali kutoa hati hiyo, lakini TFF imetoa sharti la kuitaka timu hiyo ndani ya siku 30 baada ya kupokea ITC, ihakikishe inalipa fedha za kuendeleza mfuko wa timu, ambazo ni asilimia 5 za uhamisho wake kwenda kwa timu ambazo mshambuliaji huyo alipitia.

Akizungumza Dar es Salam jana, Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura alisema wamepokea maombi ya ITC ya Samatta, ambayo tayari wameshaituma Congo.

"Tulipokea maombi hayo na pia si Samatta tu, ikumbukwe hata Patrick Ochan naye hakuombewa hivyo wameomba ITC mbili za wachezaji hao na tayari tumeshazituma, hivyo wanaweza kucheza michuano yoyote," alisema Wambura na kuongeza;

"Lakini kwa upande wake Samatta, pamoja na kutolewa kwa ITC yake kama sheria za FIFA vinavyoekekeza katika kifungu cha nne cha utaratibu wa uhamisho, bado TP Mazembe wana deni kwa upande wa timu ambazo mchezaji huyo alipitia," alisema.

Alisema kutokana na hilo wanatakiwa kulipa asilimia tano ya mfuko wa kuendesha timu alizopitia ndani ya siku 30, baada ya kupokea hati ya Samatta, vinginevyo wakishindwa kufanya hivyo kwa wakati watachukua hatua itakayostahili.

Wambura alisema fedha hizo, zitakwenda kwa timu ya Kimbangulile na Mbagala Market ambayo sasa ni African Lyon ambapo fedha hizo zitagawanywa kulingana na jinsi sheria inavyoelekeza.

Samatta alijiunga na timu hiyo akitokea Simba kwa uhamisho wa zaidi ya sh. milioni 180 pamoja na Ochan, lakini kwa ada tofauti za uhamisho ambapo uhamisho huo uliweka rekodi nchini.

James Kibosho apata ulaji Twanga

Na Mwandishi Wetu

MPIGA ngoma wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta', James Kibosho, amerithi mikoba ya aliyekuwa mwimbaji wa bendi hiyo, Charles Gabriel 'Chaz Baba' aliyetangaza kujiengua wiki hii na kuhamia Mashujaa Musica.

Mmoja wa wanamuziki nguli wa Twanga Pepeta, Khamis Kayumbu 'Amigolas' juzi usiku alimtangaza Kibosho kuwa ndiye kiongozi wa kupanga muziki jukwaani (Stage Master), nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Chaz Baba.

Tangazo hilo la Amigolas, lilipokewa kwa hoi hoi, nderemo na vifijo kutoka kwa mashabiki wa Twanga Pepeta waliofika katika Ukumbi wa Maisha Klabu, Dar es Salaam.

Twanga Pepeta hivi sasa inatamba na albamu yake ya 11 ya Dunia Daraja yenye nyimbo za Kauli, Kiapo cha Mapenzi, Umenivika Umasikini, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja na Penzi la Shemeji.

Albamu zilizopita za bendi hiyo ni Kisa cha Mpemba (1999), Jirani (2000), Fainali Uzeeni (2001), Chuki Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu Pesa (2004), Safari 2005 (2005), Password (2006), Mtaa wa Kwanza (2007) na Mwana Dar es Salaam (2009).

13 January 2012

WATU watatu wamefariki jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti

Na Zena Mohamed

WATU watatu wamefariki jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti,likiwemo la watoto Swahiba Mussa (6) na Salima Rashid (5),wakazi wa Mbweni Teta kutumbukia kwenye kisima  cha maji cha asili.
Na Rehema Mohamed

WANAFUNZI wanne kati ya 50 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wanaokabiliwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kudaiwa kujihusisha na fujo chuoni hapo wamekosa dhamana baada uongozi wa chuo hicho kujivua kuwadhamini.

Ulinzi Shirikishi

Na David John

JESHI la Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke limesema kuwa katika kuimarisha suala zima la Ulinzi shirikishi limukusudia kuazisha Uperesheni fufua, imarisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili kupambana na uharifu.

Wakuu wa miradi wapigwa msasa

Na Pamela Mollel,
Arusha

SERIKALI imeazimia kuboresha mfumo wa usimamizi wa fedha za umma na kutekeleza mipango iliyojiwekea kikamilifu ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho makubwa kupitia mfumo wa fedha(IMFS) ili kupunguza changamoto zilizojitokeza kwa miaka kumi ya utekelezaji wa mfumo wa 'Epicor 9.05' kwenye
baadhi  halmashauri  zake.

Kijiji kutumia mil 60/- kujenga zahanati

Na Thomas Kiani
Singida

UJENZI wa Zahanati ya kisasa katika Kijiji cha Nsonga Kata ya Kaselya wilayani Iramba mkoani Singida unahitaji sh. milioni 60 pamoja na nguvu kazi ya wakazi wa eneo hilo na serikali.

Wafanyabiashara waomba mfumo wa ushuru

Na Damiano Mkumbo
Singida

WAFANYABIASHARA wa mji wa Singida wameishauri Halmashauri ya Manispaa hiyo kuwapa mfumo mzuri wa kukusanyaji wa ushuru mbalimbali ili kuondoa usumbufu.

Chama cha ushirika chatoa mkopo mil 572.4/-

Na Damiano Mkumbo
Singida

CHAMA cha Ushirika wa Akiba na mikopo cha Tumaini Manyoni mjini kimetoa mikopo yenye thamani  ya zaidi ya shilingi milioni 572.4 kwa wanachama wake katika kipindi cha kuanzia mwaka 2004 na 2011.

BONDIA Karama Nyilawila aibuka

Na Mwali Ibrahim

BONDIA Karama Nyilawila ameibuka na kudai kitendo cha kunyang'anywa mkanda wake wa ubingwa wa Dunia wa WBF, na waandaaji wa mashindano hayo hakimsumbui kwani yeye anachoa angalia ni pesa.

WANANCHI wa Jimbo la Newala mkoani Mtwara

Na Rachel Balama

WANANCHI wa Jimbo la Newala mkoani Mtwara  wameomba kupatiwa elimu kuhusu ununuzi wa hisa ili wapate ufahamu na kuweza kununua hisa hizo kutoka katika benki ya Wananchi wa Newala iliyoanzishwa hivi karibuni.

Athali za Mfumuko wa Bei

Na Makumba Mwemezi

Mwaka 2012 huwenda ukawa mgumu zaidi kwa watanzania hasa wenye kipato cha chini, kutokana na Serikali kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao umepelekea benki za biashara kupandisha viwango vya riba za mikopo kutoka wastani wa asilimia 23 Mwishoni mwa mwaka jana hadi wastani wa asilimia 45 kuanzia Januari Mwaka huu.

Athali za Mfumuko wa Bei

Na Makumba Mwemezi

Mwaka 2012 huwenda ukawa mgumu zaidi kwa watanzania hasa wenye kipato cha chini, kutokana na Serikali kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao umepelekea benki za biashara kupandisha viwango vya riba za mikopo kutoka wastani wa asilimia 23 Mwishoni mwa mwaka jana hadi wastani wa asilimia 45 kuanzia Januari Mwaka huu.

Naipongeza serikali kuruhuru wanafunzi kurudia mitihani

Na Rachel Balama

DESEMBA 14, mwaka jana serikali ilitangaza matokeo ya darasa la saba ambayo kati ya wanafunzi 983,545 waliofanya mtihani huo, 567,767 sawa na asilimia 58.28 walifaulu huku  ikifuta matokeo ya watahiniwa 9,736.

BONDIA Maneno Osward 'Mtambo wa gongo'

Na Mwali Ibrahim

BONDIA Maneno Osward 'Mtambo wa gongo' amesema kuwa pambano lake kati ya Nasib Ismail litakalokuwa miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika Francis Cheka na Kalama Nyilawila ndio litatumika kuwa mazoezi ya kumuadhibu Rashid Matumla.

Maneno na Matumla wanatarajia kupanda ulingoni Februari 25 katika pambano la marudiano litakalofanyika katika ukumbi wa PTA, Saba saba Dar es Salaam.

Mabondia hao wanarudiana baada ya kushindwa kutambiana katika pambano lao lisilo la ubingwa lilofanyika sikukuu ya Krismas, Mtonikijichi ambapo Maneno hakuridhishwa na matokeo hayo ya Droo ambapo pambano hilo litakuwa ni pambano lao la nne.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Maneno alisema pambano hilo la Janurai 28 litakuwa ni sehemu ya kuonyesha kiwango chake kwani hata bondia huyo atahakikisha anamtwanga vilivyo.

Alisema, kwa sasa anaendelea na mazoezi katika kambi yake iliyopo katika ukumbi wa kwa Rich uliopo Kongowe chini ya kocha wake Chaurembo Palasa ambaye nae atakuwa ni mmoja kati ya mabondia watakao wasindikiza Cheka na Nyilawila.

Mapambano ya utangulizi katika pambano lao hilo yatakuwa ni kati ya Mikidadi Abdalah na Shomari Mirundi, Abdalah Mohamed akiwa na Salehe Mkalekwa.

Katibu mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Na Goodluck Hongo

Katibu mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stargomena Tax. amekanusha madai  yaliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Tanzania haitaki kuwa na mtangamano kuhusu uharakishwaji wa uundwaji wa shirikisho la kisiasa la Afrika ya Mashariki

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Dkt. Tax alisema si kweli hata kidogo kwamba Tanzania haitaki kuwa na utengamano na jumuiya ya Afrika ya Mashariki na kwamba lawama hizi hazina msingi kwani nchi yetu inaamini jumuiya ina faida nyingi kuliko hasara

Alisema serikali imekuwa ikisisitiza  kuwa mtangamano sharti uende hatua kwa hatua kama ilivyoainishwa katika  mkataba wa uanzishwaji wa jumuiaya katika ibara ya 5 kifungu cha kwanza

Kwa msingi huo sharti kuimarisha na kutekeleza kikamilifu umoja wa forodha na soko la pamoja; na wakati huo huo kukamilisha majadiliano ya uanzishwaji wa umoja wa fedha.Hapa ndipo tutakapoweza kusema tuko tayari kujadiliana jinsi ya kuanzisha shirikisho la kisiasa

"Serikali yetu iko makini katika kutetea na kulinda  maslahi ya wananchi wake na  katika majadiliano yoyote ya mtangamano kama ambavyo nchi nyingine wanachama wa jumuiaya ya Afrika Mashariki wanavyolinda na kuteteta maslahi ya wananchi wake " alisema Dkt Tax.


Akizungumzia uhuru wa raia wa shirikisho la  Afrika Mashariki kufanya kazi katika nchi nyingine alisema ibara ya kumi ya itifaki ya soko la pamoja inawahakikishia raia wa nchi wanachama kupata ajira katika nchi yoyote mwananchama.

Dkt Tax alizitaja baadhi ya fursa zitakazo patikana kuwa pamoja na walimu wa vyuo vya elimu ya juu, vyuo vikuu wenye shahada ya uzamivu kuanzia mwaka 2010,walimu wa shule za sekondari katika fani ya hisabati,fuzikia,baiolojia,walimu wa lugha za kigeni,walimu wa vyuo vya kilimo,ufundi stadi wenye kiwango cha elimu ya shahada ya pili katika fani husika.

Fursa zingine ni  wahandisi wa madini,majengo,maafisa ugani katika sekta ya kilimo,wauguzi na wakunga ,kada ya waongoza ndege na kada ya upimaji ramani na kuwataka watanzania kuacha hofu juu ya shirikisho hilo kwa kuwa hata watanzania wengine wanafanyakazi katika nchi hizo za jumuiya kwa kufuata vigezo na masharti ya nchi husika na fursa zote hizi zimezingatia kuwa sekta hizo zinaupungufu wa wataalamu hao.


Akizungumzia uazishwaji wa sarafu moja ya Jumuiaya hiyo alisema mchakato wa ukusanyaji maoni unaendelea na zoezi hilo linaangaliwa kwa upana wake siyo kukurupuka katika kufanya maamuzi.
Alisema kuwa inapofikia hatua hiyo lazima pawepo na usawa katika nyanja ya uchumi , viwango vya kubadilisha fedha za kigeni, na baada ya kukamilika kwa hayo ndiyo nchi wananchama wanaweza kufikia maamuzi ya kuazisha sarafu ya pamoja.

CHAMA cha mchezo wa Judo Tanzania (JATA)

Na Mwali Ibrahim

CHAMA cha mchezo wa Judo Tanzania (JATA) leo kinatarajia kupanga tarehe mpya ya uchaguzi mkuu wa chama hicho katika kikao cha pamoja na Baraza la Michezo Tanzania (BMT)

Mafunzo ya kujiepusha na madawa ya kulevya

Na Zena Mohamed

WANAFUNZI wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Chang'ombe Wilaya temeke jijini Dar es Salaam wamepewa elimu jinsi ya  kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya na  mtalaam wa  somo la stadi za maisha Bw.Yuki Koga  kutoka nchini Japan.

BENKI Kuu ya Tanzania (BOT)

BENKI Kuu ya Tanzania(BOT) imetakiwa kujiridhisha kuwa benki zilizopo nchini zinafanya biashara halali na siyo na kutunza fedha haramu.

Hayo yamebanishwa jana jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu hazina,Bw. Laston  Msongole wakati wa semina ya kuwapatia ufahamu wa athari zitokanazo na biashara ya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi ambayo huathiri uchumi wan chi husika.

Bw.Msongole alisema kuwa  vyombo vya dola vikiwemo polisi, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa PCCB pamoja na mamlaka ya mapato Tanzania TRA  vimepewa changamoto nyingi katika mapambano dhidi ya biashara hiyo haramu.

Alisema kuwa  biashara hiyo mbali na kuathiri uchumi wa taifa pia imekuwa ikisababisha kushamili kwa wimbi la uhalifu si Tanzania tu bali ni kwa dunia nzima.

Aliongeza kuwa, shughuli hizo ni za jinai na hazina tija kwa nchi yoyote kwa kuwa ni changamoto hivyo nguvu ya pamoja inahitajika ili kufanikisha vita hiyo.

Shughuli hizo haramu ambazo hufanyika nje ya mkondo halali wa mzunguko wa kifedha kutokana na wahusika kuhofia kubainika maovu yao.

"Miongoni mwa shughuli zinazopelekea kuwepo kwa fedha haramu ni pamoja na uuzaji wa dawa za kulevya, uuzaji wa silaha, rushwa na shughuli za ujambazi"alisema Bw.Msongole

"Unajuwa hii biashara ya fedha haramu imekuwa ikichangia kuporomoka kwa utawala bora na sheria, kuyumba kwa sekta ya fedha ambayo hupelekea uchumi kuporomoka, kuporomoka ushindani na kufukuza wawekezaji"aliongeza

Pia alisema kuwa michezo ya kamali ambayo huchezwa kwenye club za usiku hutumika kama njia halali ya kupitishia fedha chafu kwenye mzunguko halali wa kifedha.

"Watanzania  muwe mnatoa taarifa kwa vyombo vya dola na mamlaka husika pindi mnawapobaini  watu  mwenye utajiri mkubwa tofauti na vipato vyao ili uchunguzi ufanyike kwa ajili ya kubaini chanzo cha mapato vyao"alisisitiza

Biashara ya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi,ilianza miaka mingi lakini mwaka 2001 mara baada ya majengo ya biashara ya Marekani (WTO) kushambuliwa na magaidi wa kikundi cha Al-Qaida,nchi mbalimbali zilioanza kuitumia sheria ya kupinga biashara hiyo ambapo Tanzania ilianza rasmi kuitumia mwaka 2006 baada ya kuundwa kwa kitengo cha kushughulikia biashara hiyo kilichopo ndani ya Wizara ya Fedha.

PROMOTA kwenda mahakamani.

PROMOTA wa pamabano kati ya Francis Cheka na Karama Nyilawila Philemon Kiyando 'Don King' amesema yuko tayari kuwaburuza mahakamani Shirikisho la masumbwi Tanzania (PST) kama litasitisha pambano hilo.

sambamba na kuwaburuza mahakamani pia ataomba shirikisho hilo lifungiwe kutokana na kutomtendea haki kwa kumtaka Nyilawila kutokucheza pambano hilo ikiwa tayari ameishatumia gharama nyingi kuliandaa hadi sasa na kutaka kulisitisha wakati siku zimekaribia.

pambano hilo limepangwa kufanyika Januari 28 katika uwanja wa Jamuhuri, Morogoro likiwa katika uzito wa kg 72 raundi 12 lisilo la ubingwa.

Wakati mabondia wakiendelea kujifua Rais wa PST Emmanuel Mlundwa alitangaza pambano hilo kutokuwepo kutokana na Nyilawila kutakiwa kutetea ubingwa wake wa WBF nchini Ujeruman Februari 11 dhidi ya Mjeruman Erims Cagri.

Akizungumza na Majira Promota huyo alisema ameishatumia pesa nyingi sana kuandaa pambano hilo na tayari ameishalipia uwanja huo kwa ajili ya pambano itakuwaje liahirishwe bila kufahamishwa mapema kabla ajatumia gharama zote.

"Nimelipa mabondia, uwanja na nimeishafanya maandalizi makubwa sasa itakuwaje niahirishwiwe pambano hilo na nani tanilipa gharama zangu? mimi siwaelewi nanipotayari kuwapeleka mahakamani kwakunitia hasara kiasi kikubwa na wala sitahirisha pambano," alisema Kyando.

Alisema, kama wataweza waahirishe pamabano lao lakini pambano lake lipo palepale kama wataweza wamrudishie gharama zake zote alizotumia.

Alisema, wakati wote anaandaa pambano hilo ajapewa taarifa yoyote na PST hata kwa maandishi yeye amekuwa tu akiona kwa vyombo vya habari sasa kama ni msimamizi mzuri kwanini asimwite au amtumie barua ili asitishe maandalizi hayo.

Promota huyo alisema, yeye kama mdau wa michezo asingeweza kung'ang'ania Nyilawila acheze pmabano hilo kama tayari anapambano la kutetea ubingwa lakini bondia huyo alimfata na kumtaka amuandalie pambano kutokana na kukaa muda mrefu bila kupanda ulingoni kitu ambacho sio kizuri kwa mabondia.

"Nyilawila alikaa miezi 18 bila kupanda ulingoni na akaamua kuniomba nimuandalie nikaamua kumuandalia sasa iwaje gharama zote za maandalizi zitoke kwangu alafu ndio akatetee ubingwa huo mimi sikubali hata kidogo wao walikuwa wakimzungusha kumuandalia nimetumia gharama ndio wapitie mgongo uwo haiwezekani," alisema Kyando.

Kukaa muda mrefu kunamchangia kumshusha kiwango bondia na hasa ukizingantia anaenda kutetea ubingwa si atapigwa sana kwani hana mazoezi na mazoezi ya ndani tu hayamsaidii.

Alisema, pambano hilo pia lingemsaidia Nyilawila kufanya vyema kwani kama amekaa muda mrefu bila kupanda ulingoni hivyo angeweza kukutana na Cheka ingemsaidia kumpastamina na hata kuweza kutetea vyema mkanda wake huo.

Alisema, PST hawana utaratibu mzuri kwani wanawakandamiza  mapromota wa Tanzania na hiyo inachangiwa na wivu na chuki badala ya kushirikiana na mapromota kwa ajili ya kukuza michezo kwa ajili ya kuwainua mabondia wa hapa nchini kwani hata mapambano ya nje wanayoenda kupigania wanalipwa kiasi kidogo cha fedha tofauti na hapa nyumbani.

"Hapa kunafitina fukani kwani hata mwaka 2006 ilishawahi kunitokea nikaamua kukaa kimya na kuacha kuandaa mapambano lakini Nyilawila alivyoniomba nikaamua kurudi tena," alisema.

Lakini kwa upande wa Nyilawila amedai hatoweza kupanda ulingoni kucheza pambano hilo na Cheka kama alivyoamriwa na PST ambao ndio wanamsimamia katika pambano lake hilo la nje.

Timu 30 za mchezo wa Darts

JUMLA ya timu 30 za mchezo wa darts zinatarajia kuchuana leo katika mashindano ya taifa ya mchezo huo yanayotarajia kufanyika katika ukumbi wa Rose Garden uliopo Area C, Dodoma.