21 March 2012

Mtibwa Sugar, Simba zaingiza mil. 31/-

Na Amina Athumani
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na Simba iliyochezwa Machi 18 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro imeingiza sh. milioni 31,230,000.
Akitangaza mapato hayo Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema jumla ya watazamaji 10,410 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.

Alisema baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambayo ni sh. 4,763,898.31 kila timu ilipata sh. 6,508,230.51, uwanja sh. 2,169,410.17.

Wambura alisema Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) sh. 867,764.07, na TFF sh. 2,169,410.17.

Alisema Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,084,705.08, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 216,941.02 na asilimia 10 ya gharama za mechi sh. 2,169,410.17.

Wambura alisema gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi sh. 120,000 na tiketi sh. 2,480,000.

Alisema gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 728,700 wakati MRFA ilipata sh. 624,600..



No comments:

Post a Comment