23 March 2012

Kesi ya Lembeli yatupwa kapuni

Na Patrick Mabula, Shinyanga
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kahama imetupilia mbali mashtaka ya kesi ya madai ya sh. milioni 100 iliyokuwa inamkabili Mbunge wa Jimbo la Kahama, Bw.James Lembeli kwa tuhuma ya kumtolea lugha chafu mfanyabiashara mmoja mjini hapa.
Kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa na mfanyabiashara, Bw.Spilaus Binjampola mwaka jana  dhidi ya Bw.Lembeli alimtuhumu kuwa katika mkutano wake wa hadhara kuwa alimtolea lugha chafu wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Nyihongo mjini Kahama.

Hata hivyo katika madai yake dhidi ya, Bw.Lembeli kwenye mahakama hiyo mfanyabiashara huyo alidai katika mkutano wake wa hadahara uliokuwa ukifanyika katika viwanja vya Bwawani ndani ya kata hiyo majira ya jioni mara baada ya Mbunge Lembeli kumtolea maneno hayo alimvunjia heshima.

Bw. Lembeli alidaiwa kutoa lugha hiyo Sepemba 5, mwaka 2011 akiwa anatumia vipaza sauti katika mkutano huo ambao alikuwa anazungumza na wapiga kura wake.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo ya madai ya sh. milioni 100 katika mahakama hiyo, Hakimu mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukombe, Bi.Ushindi Swalo alitupilia mbali kesi hiyo.

Bi.Swalo alisema mbele ya mahakama hiyo kuwa uliotolewa dhidi ya mdaiwa Mbunge wa Jimbo la Kahama, Bw.Lembeli juu ya kutoa lugha chafu kwa mfanyabiashara Bw. Bijampola haukutosheleza na hivyo mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo ya madai.

Aidha, chanzo cha kesi hiyo kilitokana na eneo la wazi la Serikali lililopo katika bwawa la maji kwenye Kata ya Nyihogo mjini hapa ambalo lilikuwa bustani ya Gereza la Kahama ambalo wananchi walikuwa wakipinga kulichukua kinyemela mfanyabiashara huyo, ndipo walipomweleza Mbunge wao Bw.Lembeli ambaye naye aliungana nao kupiga kitendo hicho alichokuwa akisema ni ufisadi.

No comments:

Post a Comment