Na Mwandishi Wetu,
SAKATA la kukamatwa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania (ACT), Dkt. Valentino Mokiwa,umechukua sura mpya baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba
jalada la kesi hiyo imehitishwa Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo hata hivyo hazikuthibitishwa zilidai kuwa jalada hilo limeitwa kwa ajili ya kupitiwa kabla ya hatua zaidi.
habari hizo zilizogaa mjini hapa zilianzia Kanisa la Angilikana la Mtakatifu James jijini hapa huku kiongozi moja wa juu kutajwa kushiriki suala hilo.
Hata hivyo taarifa hizo zilitofautiana na msimamo wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha zilizoeleza kuwa zoezi hilo limekumbwa na ugumu kiasi lakini utekelezaji wake utafanyika kwa kuwa ni amri halali wa mahakama.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina wala cheo chake, mmoja wa Ofisa wa mahakama hiyo aliiambia Majira kuwa licha ya ugumu uliolikumba zoezi hilo hakuna atakayezuia sheria isichukue mkondo wake.
“Nawahakikishia kuwa sheria itachukua mkondo wake iwe leo ama siku zijazo… hakuna atakayezuia sheria isitekelezeke,”alisema Ofisa huyo kwa msisitizo bila kufafanua iwapo hati hiyo itatolewa lini wala sababu za kucheleweshwa kwake.
Kwa upande wao Jeshi la Polisi mkoani hapa limesisitiza kuwa hadi jana jioni lilikuwa halijapata hati hiyo pamoja na maamuzi juu ya amri hiyo.
Jeshihilo lilisitiza kuwa haliwezi kufanya kazi kwa taarifa zisizo rasmi hadi watakapopokea hati hiyo waichunguze na kujiridhisha ndipo watakapoitekeleza.
Kaimu Mkuu wa upelekezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha (RCO) Bw. Faustine Mafwele, kwa niaba ya Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Bw. Akilimali Mpwapwa, alisema hadi jana jioni bado hawajapata hati yoyote na kwamba wanasubiria itakapowafikia wataanza
kazi yao.
“Hadi sasa hatujapata hiyo hati, tulichosikia ni amri hiyo kupitia vyombo
vya habari tu na sisi kamwe hatufanyi kazi kupitia vyombo vya habari tu, tunafanya kazi kupitia mfumo rasmi,”alisisitiza.
Mahakama hiyo Jumatatu iliyopita iliamuru kukamatwa kwa ma Askofu Mokiwa na Stanley Hotay, kwa madai ya kukiuka amri halali ya mahakama.
Amri hiyo iliyowataka kutoendelea na shughuli zozote zinazomhusu kusimikwa kwa Askofu Hotay kuongoza Dayosisi ya Mlima Kilimanjaro baada ya badhi ya watu kufungua kesi dhidi ya suala hilo.
Waliofungua kasi ni waumini watatu wa kanisa hilo kutoka Parish ya Mtakatifu James ambao ni Bw. Lothi Oilevo, Bw. Godfrey Mhone na Bw. Frank Jackob.
.
NDIO MAANA NCHI NYINGI DUNIANI KUNA SEPARATION OF CHURCH AND STATE, MAMBO YA KANISANI NI KANISA NA MAMBO YA SERIKALI NI YA SERIKALI. HII MAMBO YA MAHAKAMA KULIAMBIA KANISA NINI CHA KUFANYA NI MAMBO YA AJABU NA INABIDI KUKOMA, MAMBO YA KANISA YAACHWE YAMALIZIKIE KANISANI.
ReplyDeleteya kaisari mwachie kaisari ya mwenyezi mwachie mwenyezi
ReplyDeleteHaaaaaaaaaaaaaa! inachekesha tena inaburudisha na mbaya zaidi inasikitisha kuona eti gharama za watanzania zinahusika na maswala ya kidini ambayo hayana faida hata kidogo. We serikali chezwa na machale katika hili, ohhhhhhhhhhhhhhhh shauri yako!
ReplyDeletendg mh.mkuu wa nchi hebu tulia sehem peke yako na ulitafakari swala hili kwa umakini mie nipo nawe kiimani ila ushauri wangu nikwamba kati ya mambo mabaya katika taifa lolote dunian ni kuingilia masuala yanayousu iman za watu!hivyo ndg yangu chochonde najua unanafasi juu ya hili,waamuru wasililete mahakamani ata kwa namna yoyote ile kwani litagawa tyaifa letu bure!na kwa sababu tuna nguvu bungeni amuru bunge liondoe mambo yote yanayousu imani kisheria yasizungumzwe katika muhimili wowote katika taifa letu!labda yale ambayo hayatagusa imani ya mtu!mie nadhan niwakati wako wa kusawazisha mabonde ya mwaka jana kwakukaa nao na sio kuongeza nyufa zile ndg yangu!na wala usiseme eti sinajiaandaa kustaafu!hapana ndg nchi inabidi ikukumbuke kwa mema zaidi!ninaandika humu kwani sina maala pengine napoweza kukuandikia ingawa sijui kama utafanikiwa kuisoma ila hata mbele ya Mungu nitakuwa huru kuhusu hili!!!Mungu akubariki katika kutatua hili na mengine mengi,kaz njema na amini tuko pamoja and wll never leave you alone hon.
ReplyDeleteNdg yangu JK jamaa wanataka kukuharibia kwa vile wewe ni nanii waseme unauchukia msalaba, cha moto utakiona.Najua huyo Said nanii akiambiwa tu amkamate moki kesho atamkamata then watu wa nanii wataku mind ile mbaya. Zuia hiyo kitu wenzio hawakufanya hayo hangaika na akina Masilaha na Mbwe au Ziito wepesi wepesi.
ReplyDelete