16 June 2011

CHADEMA wamethibitisha uongo wao-Nape

Na Charles  Masyeba

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Nape Nnauye, ameponda bajeti ya kambi ya upinzani iliyowasilishwa bungeni jana kudai kuwa ni
kielelezo cha uwongo wa kambi hiyo.

Bajeti hiyo iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri kivuli wa Fedha Bw. Zitto Kabwe, pamoja na mambo mengine ilitoa aueni karibu kwa kila kundi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Bw.Nnauye alisema kimsingi bajeti hiyo imeacha maswali mengi yasiyo na majibu.

Alisema Chadema iliahidi wakati wa kampeni kuwa itatoa elimu bure kwa watanzania kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu lakini bajeti yao inasema wataondoa ada kwa wanafunzi wa kutwa wa shule za Sekondari na kupunguza ada kwa Sekondari za bweni kwa kiwango cha asilimia 50.

Alisema bajeti hiyo ilitoa aueni wavulana kwa asilimia 50 na wasichana kusoma bure kinyume na walivyoahidi kwenye kampeni.

Alisema bajeti hiyo mbadala haina mpango kuhusu elimu ya juu na kwamba wanakiri na kukubali kuwa serikali haiwezi kutoa elimu bure.

Alisema wameahidi kuongeza kima cha chini cha mshahara kufikia shilingi 315,000/- kwa mwezi na kutoa motisha kwa walimu wanaofundisha vijijini bila kuonyesha mchanganuo wa mapato ya fedha hizo.

Kiongozi huyo wa CCM alisema wakati wanalalamika kuwepo kwa wakwepa kodi na kutaka kila mtanzania mwenye kipato alipe kodi wao wanaendelea kumlipa Katibu wao Mkuu Dkt. Wilbroad Slaa, zaidi ya shilingi milioni saba ambazo hazikatwi kodi yoyote.

Alisema bajeti ni zao la ilani ya uchaguzi ya chama husika hivyo sasa imedhihirika kuwa maneno mengi na ahadi zilizotolewa na Chadema wakati wa kampeni katika uchaguzi Mkuu mwaka jana zilikuwa ahadi hewa na ghiriba kwa wananchi.

10 comments:

  1. Kwani CHADEMA ndiyo yenye dola? Naona CCM imekuwa Chama cha upinzani ssa. Pia madai ya Nape hayana ukweli, kwani Ilani ni kitu cha miaka mitano, na Budget ni ya mwaka mmoja. Kupunguza ada kwa 50% wavulana shule za boding na kufuta ada kwa wasichana boding na wanafunzi wote wa kutwa ni hatua kubwa sana. Pia kuondoa kodi kutapunguza bei za bidhaaa. Kufuta misamaha ya kodi na posho kutalisaidia Taifa kuongeza kipato na kuwezesha kupandisha kima cha chini cha mshahara pamoja na kufanikisha shughuli za maendeleo. Hii Tanzania ya leo si ya kuendeshwa kwa Propaganda, nashauri CCM wafute kitengo hiki kabisaaa.

    ReplyDelete
  2. nape ana lake jambo , mwanaccj huyo, hata ccm wakifanya jambo zuri mbona tunawasifia ?, wao ccm sera zao kuu ni kupinga kila jambo la upinzani hata liwe zuri na wizi basi.

    ReplyDelete
  3. ama kweli kupenda kubaya, maana ukipenda mno CHONGO utasema KENGEZA

    Nape kafafanua vema sana, lkn watu wameshapenda hata km wakiwekewa mikuki ya moto shingoni kwa uongo wa CHADEMA bado watasema CHADEMA wazuri. Somo kila mstari wa maoni ya CCM kisaho someni hiyo Bajeti mbadala ndipo mchangie.

    wenye akilia timamu hawamjadili mtu wanajadili hoja zake

    Sasa kama Mnasema CCM kupitia Katibu wake Mwenezi wamekosea kuichambua hiyo Bajeti ya Kambi ya Upinzani, nyie toeni maoni msingi ukiwa kujibu hoja na siyo kumsema mtu

    ReplyDelete
  4. Nape hana kitu, sijui elimu yake ni ya darasa la ngapi, ndiyo maana alitusaliti akaenda kuanza chama chake. Ni mnafiki mvivu kufikiria na ni mtu mwenye dhamira ya kulipa kisasi tu hata kama tutampa madaraka makubwa zaidi ya haya ya umbea wa chama tuliyompa. Tunataka CCM mpya yenye mtazamo chanya kama wa wawapinzani, usiwe kama ndumi la kuwili, huku unataka,kule unataka utabakia njia panda. Jaribu kutafakari kabla hujaongea, mambo ya ufisadi ya akina Rostam, Lowasa yameishia wapi, leo unaamka na kukurupuka tu hujui chochote.....

    ReplyDelete
  5. We ndo unapenda vbaya..NAPE SOMA VZR BAJET YA UPINZAN MAJIBU YA MASWAL YAKO YOTE yapo humo..acha kujidharirisha Dr.SLAA AJIKATE KOD MWENYEWE?SERIKAL YA CCM NDO ILIYOWEKA SHERIA POSHO HAILIPIW KOD..SA KOSA LAKE LIPO WP?DR.ATAENDELEA KUTOKUKATWA KOD HADI HAPO SHERIA ITAKAPOBADILISHWA na hata acha kupigia kelele kuhusu ukusanyaji wa kodi kamwe..wewe kwel ccj yan mambo unayoyatamka ni kuiua ccm kaz nzur sana

    ReplyDelete
  6. Nape ahad za jk zpo kwenye bajet?barabara za angan vp cjaona..meli, ndege, bajaji, n.k. Afu kulikuwa na vipaumbele kumi na mbil mbona sa iv vimekuwa vitano?tehe tehe tehe..siasa bana kwan chadema wanaongoza nch?wapen muone..kwan ilan ndo bajet nape? We kwel kilaza unatia kinyaa

    ReplyDelete
  7. Changa la Macho, kwanza sihitaji hata hiyo Bajeti Mbadala hainisaidii kitu ni kama Bendera inafuata Upepo, Bajeti simchezo wala Mzaha. Chadema bado tena bado sana siwezi kuanza kuwachambua kwa sasa lakini hiyo Bajeti ni kiini macho,Uongo na Upuuzi mtupu. tuache longolongo kwenye masuala ya Msingi. Nimabingwa wa Uchochezi, Migomo na Maandamano. Kwenye Bajeti Mbadala Mmetereza.

    ReplyDelete
  8. Nape subiri yakwako yako jikoni wewe si unataka mapacha watatu waondoke basi nakuambia utaondoka nao kwani wewe ni msaliti mkubwa na CCJ yako. La sivyo mtawacha na utalaumiwa na uma kwaahadi ya kujivua gamba vipi yahe utakuma. Hapo ulipo ujiweka pabaya.

    ReplyDelete
  9. Jamani nataka kujua elimu ya Nape, mbona anachokiandika inaonekana elimu yake ndogo sana. samahani siyo elimu tu bali hata uelewa wake naona mdogo sana.
    Mbona anashindwa kujenga hoja. Hivi CCM hakuna wanoelewa? yanini muache mtu anayezalilisha chama?

    ReplyDelete
  10. IMEFIKANA WAKATI WATZ KUCHAMBUA MAMBO KWA KINA. TUNAKUSHUKURU NAPE KWA KUONA HAYA MAMBO NA KUWAFAFANULIA WANANCHI. GHIRIBA ZA NAMNA HII ZA CHADEMA WATANZANIA WAANZE KUONA. WANACHOHUBIRI SIYO WANACHOISHI .

    ReplyDelete